Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, January 25, 2016

UPDATES: ESTER BULAYA (CHADEMA) AIBUKA MSHINDI MAHAKAMANI LEO


Mahakama kuu kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya uchaguzi ya kupinga ubunge wa Bunda mjini na kumpa ushindi Ester Bulaya kutokana na walioleta maombi hawana ya kisheria kufungua kesi.
Baada ya Mahakama kutupilia mbali kesi hiyo Mbunge huyo wa Bunda Mjini Ester Bulaya kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook ameandika maneno haya 

 
"Nilimshinda Wasira kwa wananchi, na leo nimemshinda kisheria, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya Uchaguzi dhidi yangu, iliyofunguliwa na wapambe wa wasira. Mungu husimama na watu waliowema. Nakutumaini mungu wangu na wewe ndiye mlinzi wangu.Asante sana Wananchi wangu wa Bunda Mjini mliokwenda Mwanza kusikiliza Hukumu. Mbunge wenu nipo dodoma tayari kwa kuanza vikao vya Bunge Kesho"

No comments:

Post a Comment