Watendaji hao sita waliosimamishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha tarehe 28.01.2016
walihusika na ubadhilifu wa fedha hizo kwa kuzitumia bila kufuata kanuni,
taratibu na sheria za kuomba idhini ya kuhamisha vifungu vya fedha au
kubadilisha matumizi yake kutoka fungu moja kwenda fungu lingine.
Hayo yalibainishwa na Kamati ya Wataalamu
sita iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Mongella katika kikao cha Bodi ya Barabara
kilichofanyika tarehe 21.01.2016 Mkoani Kagera na kuiagiza Kamati hiyo
kuchunguza upotevu wa fedha hizo
mara baada ya Mhandisi wa Halmashauri hiyo kuwasilisha taarifa ya matengenezo ya barabara na madaraja kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
mara baada ya Mhandisi wa Halmashauri hiyo kuwasilisha taarifa ya matengenezo ya barabara na madaraja kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Kamati hiyo ya wajumbe sita
iliyoongozwa na Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Sekretarieti ya Mkoa wa
Kagera Bw. Sabora Wambura na ilipewa siku tano iwe imekamilisha taarifa yake.
Aidha, taarifa ya Kamati hiyo iliwasilishwa mbele ya Mkuu wa Mkoa, Baraza la
Madiwani, Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Kamati ya Ulinzi na
Usalaama ya Mkoa na Wilaya tarehe 27.01.2016.
Katika kikao hicho cha kupokea
taarifa ya ubadhirifu wa shilingi milioni 851, Watendaji waliohusika walihojiwa
mara baada ya taarifa kuwasilishwa na kuonekana walitumia fedha hizo kinyume na
utaratibu wa fedha, katika mahojiano hayo walikiri kuwa utaratibu wa fedha
haukufuatwa na kukiri makosa yao.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Mongella mara
baada ya kuwahoji alikubaliana na Baraza la Madiwani kuwa watendaji hao
wanatakiwa kuwajibishwa na kuliagiza Baraza hilo kukaa kikao na kuamua hatua ya
kuchukua kwa wahusika wote kwani mamlaka ya kuwawajibisha Wakuu wa Idara wa halmashauri
ipo kwa Madiwani wenyewe.
Aidha, alimwagiza Katibu Tawala
Mkoa kumwadikia barua Katibu Mkuu
TAMISEMI ili aweze kumchukulia hatua Mkurugenzi Mtendaji Bi Gradis Dyamvunye
aliyekuwepo wakati huo na kuomba aliyekuwa Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri
hiyo Robert Massoro kurudishwa kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za
mfuko wa barabara pia kuomba ufanyike ukaguzi maalum mara moaja.
Kikao cha Baraza la Madiwani
kilichofanyika tarehe 28.01.2016 kikiongozwa na Mwenyekiti wake Mustapha Ngeze
kiliamua kwa kauli moja kuwasimamisha kazi kupisha uchunguzi wa upotevu wa
milioni 851 watendaji wafuatao;
Idara ya fedha ni Bw. Jonathan
Katunzi (Mweka Hazina), Selialisi Mutalemwa, Idara ya Ujenzi ni Bw. Deus Bizibu,
Elimu Sekondari ni Bw. Lucas Mzungu, Mifugo ni Dk. Kisanga Makigo na
Bw.Mustapha Sabuni ni Afisa Mipango.
Mchanganuo wa fedha zilizotumika
blia kufuata utaratibu na kanuni za fedha ni Shilingi milioni 200 za mfuko maalum wa
barabara zilizokuwa zimeletwa kwa ajili ya kujenga daraja la Kyamabale, Milioni
176 za mfuko wa barabara kwa ajili ya kutengeneza na kukarabati barabara, Milioni
168 za mfuko wa Jimbo, na Milioni 307 za mfuko wa Afya (Busket Fund)
CHANZO: BUKOBA WADAU
No comments:
Post a Comment