Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, February 1, 2016

ASKOFU DKT FREDRICK SHOO ,MKUU MPYA WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA (KKKT).

Mkuu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt Alex Malasusa akizungumza wakati wa ibada ya kumuingiza kazini mkuu mpya wa KKKT,Dkt Fredrick Shoo,ibada iliyofanyika kanisa la KKKT usharika wa Moshi mjini .
Mawaziri wakuu wastaafu,Edward Lowasa na Frederick Sumaye wakiwa katika ibada hiyo.
Waziri mkuu Mstaafu Frederick Sumaye akiwa katika ibada hiyo .

 
Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzania Bungeni na Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akiwa na mkewe katika ibada hiyo.
Mbunge wa zamani wa jimbo la Siha,Aggrey Mwanry pia alikuwa ni miongoni mwa wageni waliohudhuria hafla hiyo.
Katibu Mkuu wa LWF ,Mchungaji Martin Junge akitoa mahubiri wakati wa ibada ya kuingizwa kazini kwa mkuu mpya wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ,KKKT ,Dkt Fredrick Shoo.
Waimbaji kutoka maeneo mbalimbali pia walitoa mahubiri kwa njia ya nyimbo wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya waumini waliohudhulia ibada hiyo.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kssim Majaliwa akiwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala wakifuatilia ibada hiyo.
Kutokana na ufinyu wa nafasi katika kanisa hilo ,waumini wengine walitengewa eneo la nje kufuatilia ibada hiyo.
Ibada ya kumsimika na kumuingiza kazini ,Mkuu Mpya wa KKKT ,Dkt Fredrick Shoo ikifanyika .
Mkuu mstaafu wa KKKT,Dkt Alex Malasusa akimpongeza Mkuu Mpya wa KKKT,Dkt Fredrick Shoo mara baada ya kuingizwa kazini katika ibada maalumu iliyofanyyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Moshi mjini.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia pia likuwa ni miongoni mwa wageni waliohudhuria ibada hiyo.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akiwa na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akiwa na mkewe Anande katika ibada hiyo.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPPP,Dkt Reginald Mengi akiwa na mkewe Jackline katika ibadda hiyo.
Mkuu mpya wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania,KKKT ,Dkt Fredrick Shoo akizungumza mara baada ya kuingizwa kazini .
Askofu wa Jimbo la Moshi ,Mhashamu Baba Askofu Isack Amani Massawe akitoa salamu kwa niaba ya kanisa Katoliki katika ibada hiyo.
Waziri mkuu wa JAmhuri ya Muungano wa TAnzania ,Kassim Majaliwa akizungumza kwakati wa ibada hiyo ,akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Pombe Magufuli.
Mkuu mpya wa KKKT,Dkt Shoo akihitimisha ibada hiyo.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri mkuu Mstaafu,Edward Lowasa walipokutana katika ibada hiyo.
Mgeni rasmi katika ibada hiyo,Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na maaskofu wa KKKT.
Mkuu Mpya wa KKKT ,Dkt Shoo akipeana mkono na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala.
Baadhi ya waumini wakitoka katika kanisa hilo mara baada ya kukamilika kwa ibada ya kumuingiza kazini Mkuu mpya wa KKKT,Dkt Fredrick Shoo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment