Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, February 19, 2016

COSATO CHUMI AINGILIA KATI MVUTANO WA WAMACHNIGA NA HALIMASHAURI

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwasikiliza wafanyabiasha wadogowadogo

  wafanyabiasha wadogowadogo wakiwasikiliza Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi
NA FREDY MGUNDA,MAFINGA

Mvutano mkali kati ya wafanyabiashara wadogo  wadogo ( machinga) mjini mafinga mkoani Iringa  na uongozi wa halimashauri hiyo umeendelea kufukuta baada ya wafanyabiashara hao kugomea kuondoka katika eneo hilo wakidai maslai ya watu wachache ndio yanayowahamisha katika eneo hilo jambo lilopelekea mbunge kuingilia kati  .

Wakitoa kilio chao mbele ya mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi wafanyabiashara hao walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kwa muda mrefu na halimashauri hiyo  kwa kuhamishwa hamishwa kila kuikicha na kupelekwa maeneo ambayo siyo rafiki kwa biashara zao .

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Glibet amoni  alisema hapo awali walikuwa wakifanyia biashara zao bembeni ya soko la mafinga Uwanja wa mashuja ) na badaye kuja kuhamishwa katika eneo hilo na kupelekwa katika eneo la Kinyanambo ambalo pia halifai kwa biashara kwa kuwa kipindi cha mvua vitu vyao huzama kwenye maji kwa kuwa eneo hilo huwa linasimamisha maji pindi mvua inyeshapo .

Alisema kuwa baada ya kuona eneo hilo linaharibu biashara zao waliamua kurudi katika eneo lao la awali la mashuja na kuutaarifu uongozi wa halimashauri hiyo kuwa wamerejea katika eneo hilo  lakini walifanya biashara kwa majuma mawili na baadaye kuja kutangaziwa kuondoka katika eneo hilo na kwenda katika soko jipya ambalo pia miundombinu yake haijakamilika na wali sio eneo la wamachinga 

Alisema kuwa walishanga kusikia matangazo ya barabarani kuwa hakutakuwa na mnada katika eneo hilo siku ya jumapili na walipoenda siku hiyo walikuta magari ya polisi yakiwa yametanda katika eneo hilo kuwazuiya kufanya biashara katika eneo hili jambo lilizodii kuwadhofisha kwa kuwa wengi wao nawamikopo katika maeneo mbalimbali na wanapaswa kurejesha mikopo hiyo

“Mh mbunge wewe ndio msaada wetu uliahidi kututetea sana tunaona kuna mambo ya siasa yanaingia hapa kwani huyu mwenyekiti wa halimashauri Charles Makoga anatulazimisha kwenda kule kwa kuwa yeye anavibanda vyake kule sokoni ndio mana analazimisha tupelekwe kule  na tushanga kuja kututangazia kibabe na kuondolewa a na polisi kama vile ni majambazi wakati ushuru wao tunalipa na eneo huwa tunafanya usafi kwani wanatufanyia hivii au sisi sio watanzania ”

Waaliongeza kuwa wao siku yao ya kufanya biashara ni siku moja tu ya wiki yani jumapili lakini wameshanga kuona ungozi wa halimashauri hiyo kwa kushirikiana na wafanyabiashara wachache wa soko kuu wanaolalamika kutokuza biadha zao pindi mnada huo unapofanyika katika eneo jambo ambalo siyo la kweli.

Akipokea kilio chao mbunge huyo wa mafinga mji Cosato chumi awaliwata wafanyabiashara hao kuwa wavumilivu ili kuweza kwenda kuzungumza na uongozi wa halimashauri hiyo ili kuona ni sababu gani zilizopelekea wao kutolewa katika eneo hilo na kupelekwa soko jipya eneo ambalo limetegwa kwa ajili ya soko na wala sio kwa ajili yam nada wa siku moja .

Chumi alisema yeye kama mbunge Hata kubali kuona wananchi wake wananyanyaswa na watu wachache kwani yeye ni mbunge wa watu wote na wala hatakubali kuona watu wake wakipelekwa katika maeneo ambayo siyo rafiki kwa biashara 

‘’Kilio chenu nimekisikia na mimi nataka kukimbizana na kasi ya magufuli ya kuwatetea wanyonge sioni sababu za msingi za nyie kuhamishiwa kule soko jipya wakati nyie huwa munafanya mnada siku moja tu hao wanaosema hawauzi kwanini wanakuwa wabinafsi hivyo ase yani wao wanauza siku sita nyie mnada wenu ni siku moja  halafu eti wanasemna hawauzi mi niwambie waache ubinafsi na hili sitakubaliana nao ’’

Chumi alisema kuwa kimhesabu kupeleka mnada katika eneo hilo lililojengwa kwa kwa ajili ya soko ni kupoteza mapato ya halimashauri kwani badala ya kukusanya ushuru wa siku saba kwa wiki watakuwa wanakusanya ushuru wa mnada ambao ni siku moja kwa wiki jambo ambalo kimahesabu halikubaliki 

Kwa upande wake katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Jimsoni mhagama alisema inapaswa busara kutumika katika kuwasimamia wafanyabiashara hao na kuchana na kutumia ubabe kwani nao wanahaki ya kufanyabiashara kama wanavyofanya watu wengine .

Mhagama alisema kuwa serekali ya Raisi Magufuli ni serekali inayowangalia wafanyabiashara wadogo kwa jicho la pili ili waweze kufanikiwa katika biashara hao na kuwanyanyasa au kuwahamisha bila ya kukaa chini na kukubaliaba siyo jambo la busra na ofisi yake atajaribu kuangallia jinsi gani ya kuwasaidia ili wafikie muafaka 

No comments:

Post a Comment