Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, February 12, 2016

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION KUENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA MKOA WA ARUSHA

 Picha Wanawake kutoka Visiwani Zanzibar walionufaika na Mradi wa Manjano Dream Makers Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation..
Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi  Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers  ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Arusha kuanzia tarehe 15 Februari 2016 kwenye ukumbi wa Golden Rose Hotel, Conference Centre Arcade jijini Arusha. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake 30 kutoka mkoani Arusha na mikoa ya jirani. 
Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Arusha wanafikia 

 
malengo yao waliojiwekea. Wanawake wakazi wa Jiji la Arusha waliotuma maombi na wanaopenda kunufaika na mradi huo  wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumamosi tarehe 13 Frbruari 2016 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye hoteli ya Golden Rose, Conference Centre Arcade jijini Arusha.
Mafunzo yana lengo la  kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 
Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba ya bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 784 661 080 au +255 762 744 714

No comments:

Post a Comment