Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, February 10, 2016

TAZAMA PICHA::WACHEZAJI WA CONGO WAZAWADIWA MAGARI YA KIFAHARI BAADA YA KUCHUKUA UBINGWA WA CHAN

Wachezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamezawadiwa magari ya kifahari baada ya kushinda Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN).Rais Joseph Kabila amemtunuku kila mchezaji gari gari la kifahari la thamani ya $60,000 (£40,000).

 
Wachezaji hao pia wamepewa nishani.Chui hao wa Kinshasa walitwaa kombe kwa kulaza Mali 3-0 kwenye fainali na kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mara mbili.Mwandishi wa BBC Mbelechi Msochi anasema mchezaji Heritier Luvumbu Nzinga aliyeumia kwenye michuano hiyo pia ameahidiwa kwamba atasafirishwa ng'ambo kwa matibabu.


No comments:

Post a Comment