Mheshimiwa Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo,
Kwanza pole sana kwa majukumu mazito ya kitaifa unayoendelea nayo, na hongera sana juu ya utendaji wako uliotukuka.
Mimi mwananchi wa kata ya Mbopo wilaya ya Kinondoni, nimeona nikuandikie kukufahamisha juu ya hili la utendaji wa hovyo wa shirika la umeme TANESCO hapa tawi la TEGETA.
Mwaka 2014 Mwezi wa kumi na moja tulipata nguzo sisizopungua 84 kwa ajili ya mradi wa umeme kwenda MBOPO (Dispensary, Shule na Wananchi wa kawaida). Ni jambo tulilolifurahia sana kwa imani kuwa umeme ungefika kwetu mara moja.
Jambo la kustaajabisha baada ya hapo hali ikawa kimya. Katika kufuatilia tukaambiwa kuwa baadahi ya vifaa havijafika, tukavuta subira. Tulipata
taarifa ya kuwa vifaa vimefika hivyo wakati wowote kazi itaanza.
taarifa ya kuwa vifaa vimefika hivyo wakati wowote kazi itaanza.
Baada ya kuona muda unapita bila ya kuona kazi ikianza tukafuatilia na kuambiwa kuwa TANESCO kwa sasa hawana hela kama inawezekana tujichange tuchimbe mashimo, tukajichanga fedha isiyopungua Tsh. 1,500,000/= tukafanikisah kuchimba mashimo yote na tukasimamia uwekwaji wa nguzo zote.
Kimya kikatawala tena, tukitaka vifaa hadi tuchangie hela ya mafuta tena vije weekend. Tuakkata tamaa hadi uchaguzi ulipokwisha.
Baada ya Mh. Rais kuanza kushughulikia wazembe kazini ghafla tukaona TANESCO wamekuja na kuanza kufunga nyaya, hata kazi haijafika robo wamepotea hatujawaona tena hadi leo hii na kwa masikitiko zaidi baadhi ya nyaya zinaning'inia chini kabisa hali ambayo inaweza sababisha kuibiwa na wananchi kuibiwa.
Kweli tunahitaji umeme, ila kama TANESCO hawapo tayari kutupatia basi japo waje waweke hizi nyaya juu zisiibwe(Tizama picha).
Wewe ni mchapa kazi, ila TANESCO ni wazembe na wengi wao ni Miungu watu.
Mradi wa 2014 leo haujakamilika tukiwa na ushahidi wa sehemu hizo hizo(jirani zetu) ambazo hawakuwa na hata nguzo moja wao wamepata umeme.
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Africa.
Mimi Mwananchi.
Nawasilisha
No comments:
Post a Comment