Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwasalimia Wanachama cha Mapinduzi katika mkutano wa hadhara wa Mikoa minne ya Unguja mara alipowasili katika shamra shamra za Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Ofisi kuu
Baadhi ya Wananchi na Wanachama cha Mapinduzi (CCM) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake katika shamra shamra za Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiangalia vijana wa halaiki katika mkutano wa hadhara wa ya shamra shamra za Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi na Wanachama cha Mapinduzi katika mkutano wa hadhara wa Mikoa minne ya Unguja shamra shamra za Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar
Makamo Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa wakati alipowasili katika uwanja wa Ofisi ya CCM Kisiwandui katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM. Picha na Ikulu.
Na Ally Ndota, Zanzibar
MAKAMO
mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa miaka 39
ya kuzaliwa kwa CCM ni kilele tosha cha kupatikana kwa maendeleo katika
Nyanja mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Akizungumza
katika uziunduzi wa miaka 39 ya kuzaliwa kwa chama hicho katika viwanja
vya Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, amesema kuwa maendeleo
yaliyopatikana katika serikali zote mbili ya Tanzania bara na Zanzibar
yamesimamiwa na miongozo, ilani na mikakati mbali mbali iliyotokana na
CCM.
Dkt.
Shein alisema kuwa CCM iliyozaliwa mwaka 1977 baada ya kuungana kwa
vyama viwili vya ukombozi vikiwemo TANU na Afro shraz party (ASP), chama
hicho kimeweza kupigania haki za wanyonge kwa kusimasmisha serikali
zenye misingi imara ya kuwatumikia wananchi kwa moyo wote bila ya
ubaguzi.
“
Serikali nyingi zilizoundwa na vyama vya ukombozi duniani zimeangushwa
na wakoloni kwa njia za kiutapeli lakini sisi serikali zetu bado ni
imara na zitaendelea kutawala wananchi kwa njia bora na za kidemokrasia.
Pia ni lazima tuendelee kujitathimini kwa kila jambo nje na ndani ya
chama chetu kwani bado kuna changamoto mbali mbali zinazotakiwa
kufanyiwa kazi ipasavyo”, alisema Dkt. Shein.
Aidha
Dkt. Shein aliwasihi wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla
kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20
mwaka huu, ili wapatikane viongozi wa kuongoza dola kwa miaka mitano
ijayo.
Dkt.Shein
alifafanua kwamba msingi wa uchaguzi wa marudio upo kikatiba kwani
uchaguzi mkuu uliopita ulifutwa kisheria na mamlaka iliyokuwa inahusika
na usimamizi na uratibu wa uchaguzi huo baada ya kubaini kasoro.
Akizungumzia
mgogoro wa kisiasa uliopo visiwani Zanzibar, Dkt. Shein alisema kuwa
ulikuwa utatuliwe kwa njia za mazungumzo lakini kiongozi wa CUF ambaye
ni Maalim Seif Sharif Hamad aliyeomba mazungumzo ya maridhiano kabla
hayajamaliza yeye alienda kutoa siri za vikao kwa waandishi wa habari
Dar es saalam na baadae kuandika barua ya kujitoa katika mazungumzo
hayo.
Aidha
aliwataka wananchi kuendelea kulinda Amani na utulivu wa nchi na
kuepuka kutumiwa na baadhi ya vyama vya kisiasa kufanya vurugu
sizisokuwa na msingi kwa maslahi ya nchi.
Akizungumza
katika hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai
alisema kuwa Zanzibar CCM itaendelea kuwa chama cha wananchi wote
kinachoongozwa na uzalendo.
Alisema
kuwa mpaka sasa CCM Zanzibar imejiandaa kwa kila hatua katika kushiriki
kwenye uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment