Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, March 17, 2016

ACCESS BANK WATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM WANAOSOMA SHULE YA MSINGI MTAMBANI

Meneja Masoko wa AccessBank Mr.Muganyizi Jonas Bisheko Akikabidhi Vifaa Mbalimbali kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum wanaosoma  shule ya Msingi Mtambani Iliyopo Boko Manispaa ya Kinondoni.
Benki ya Access Bank imetoa Msaada wa Wanafunzi Wenye Mahitaji maalumu wanaosoma Shule ya Msingi Mtambani Manispaa ya Kinondoni.Meneja Masoko kutoka Access Bank alisema Msaada huo ni sehemu ya faida ya Benki hiyo Ambayo Wnarudisha kwa Jamii ya Watanzania hivyo waliguswa na Changamoto Kubwa Zinazowakabili Wanafunzi hao ikiwwemo Ukosefu wa Miundo mbinu Rafiki kwajili ya Wanafunzi hao kama Madarasa vyoo na Vitendea kazi vingine.Akieleza zaidi Bw Muganyizi Jonas Bisheko Ameomba Makampuni Mbalimbali Kujitokeza Kuwasidia wanafunzi wao wenye mahitaji Maalum kwa lengo la kuwezesha kupata elimu Bora kawa Wanafunzi wengine.Benki hiyo imetoa Vifaa mbalimbali vya kujifunzia pamoja na Michezo kwajili ya kusaidia kutatua Changamoto zinazowakabili wanafunzi hao
Msaada huo unajumuisha vitu mbalimbali ikiwemo vifaa vya kujifunzia pamoja na Michezo,akieleza zaidi Meneja Masoko wa Benki hiyo amesema 

 
Accessbenk imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii ya watanzania hasa kupitia sekta ya elimu kwa kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo kama vile ukosefu wa vifaa na mazingira rafiki ya kuwezesha kutoa elimu bora
Mwalimu wa shule ya Msingi mtambani anayehusika na Kitengo cha wanafunzi wenye Mahitaji Maalum akitoa neno la shukrani Mara baada ya Kupokea Msaada huo.Ameishukuru sana Accessbenki kwa msaada wao amesema kwa kiasi utatua Changamoto zinazowakabili wanafunzi hao.
Wanafunzi Wenye mahitaji Maalum kutoka Shule ya msingi mtambani walionufaika na msaada huo kutoka accessbenki.

No comments:

Post a Comment