Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, March 11, 2016

GOLIKIPA WA ZAMANI WA SIMBA ABEL DHAIRA ANASUMBULIWA NA SARATANI YA UTUMBO

 Abel Dhaira akiwa na kocha wake Bjarni Jóhannsson
Golikipa wa zamani wa klabu ya Simba SC, Abel Dhaira ambaye kwa sasa anachezea klabu ya IBV Vestmannaeyjar ya nchini Iceland na timu ya taifa ya Uganda, anasumbuliwa na satarani ya utumbo.
Kocha wake Bjarni Jóhannsson amesema klabu ya IBV itapitisha harambee kupitia uongozi wake ili kumsaidia Dhaira kupata fedha kwa ajili ya matibabu. Dhaira ni mtoto wa kipa nyota wa zamani wa Uganda, Bright Dhaira.

Abel Dhaira alivyo kuwa akiichezea klabu ya Simba SC
Pamoja na harambee hiyo, Jóhannsson amesema: “Ni jambo la kusikitisha, linaumiza na kushitua. Lakini bado tuungane kumuombea Abel ambaye alikuwa mpambanaji.

 
“Kama mwalimu, pamoja na wachezaji, klabu kwa ujumla tumekuwa naye pamoja katika kipindi chote cha wakati mgumu wa kuugua akiwa hapa Iceland na baadaye aliporejea Uganda. Tunawaomba wadau wote wa soka tuungane ili kumuombea na kumsaidia Abel ambaye sasa anateseka.”

Source: salehjembe

No comments:

Post a Comment