Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, March 18, 2016

MAKALLA ATAKA SUALA LA UGONJWA WA KIPINDUPINDU LIWE HISTORIA MKOANI MBEYA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mstaafu Abbasi Kandoro (kulia) akimkabidhi rasmi ofisi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Machi 17 mwaka huu.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na watumishi  waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Abaas Kandoro Machi 17 mwaka huu .


Baadhi ya watumishi wa ofisi ya mkoa wa mbeya wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa huo Amos Makalla wakati akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Abasi Kandoro Machi 17 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abbas Kandoro akizungumza na watumishi na baadhi ya viongozi (hawapo pichani)waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofsini na Mkuu wa Mkoa mpya Amosi Makalla Machi 17 mwaka huu.

Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya  wakiwa makini kumsikiliza Mkuu wa Mkoa mstaafu Abbas Kandoro wakati awaaga rasmi mara baada ya kustaafu rasmi nafasi hiyo.
Na Emanuel Madafa, Mbeya.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala,  amewaagiza watendaji wote wenye dhamana ya kulinda afya na usalama wa wananchi kuhakikisha kuwa ugonjwa wa kipindipindu unakuwa historia mkoani Mbeya kwa kusimamia usafi katika ngazi zote za kijamii.
Mbali na agizo hilo , pia Makala amewaagiza Wakuu wote wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani humo kuandaa madawati ya malalamiko katika kila siku za Alhamisi  kuanzia ili kusikiliza malalamiko ya wananchi kuhusu kero mbalimbali zinazojitokeza kwenye maeneo yao.
Mkuu huyo mpya wa Mkoa wa Mbeya  ametoa maagizo hayo katika hafla fupi ya kukabidhiwa ofisi ya mkoa wa Mbeya na mtangulizi wake, Abbas kandoro, ambaye amestaafu utumishi wa umma baada ya kufanya kazi kwa miaka 40 kuanzia mwaka 1976.
Amesema suala la ugonjwa kipindupindu hatopenda kulisikia katika uongozi wake hivyo amezitaka mamlaka husika kuwajibika ipasavyo ili kudhibiti kabisa ugonjwa huo hatari.
Wakati huo Makala amepiga marufuku matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watumishi wa umma mkoani humo, wakati wa saa za kazi ili kutoa fursa kwa watumishi hao kutimiza vyema majukumu yao kazini.
Ameonya kuwa  hatamvumilia mtumishi yeyote atakayebainika kupoteza muda mwingi kwenye mitandao hiyo huku akishindwa kutimiza majukumu yake katika kuwatumikia wananchi.
 Hata hivyo, Makala alitahadharisha kuwa haitaji majungu ya aina yoyote kutoka kwa watumishi wa sekta wala wanannchi mbalimbali mkoani hapa ili kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza majukumu yake na si kukwamishana katika  utendaji wa kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abaas Kandoro amewashukuru watumishi na viongozi mbalimbali kwa ushirikiano waliompa wakati wa utumishi wake na kuahidi kutoa ushirikiano kwa mkuu wa mkoa huo Amosi Makala  .



No comments:

Post a Comment