Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, March 1, 2016

TANZIA: KIFO CHA MZEE SELEMANI KIKWETE (KAKA WA DR JAKAYA MRISHO KIKWETE - M/KITI WA CCM TAIFA NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA 4 WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA)


Uongozi wa Shirikisho Taifa umepokea kwa masikitiko makubwa sana kifo cha Mzee Selemani Kikwete ambae ni kaka wa M/kiti wa CCM Taifa - Dr Jakaya Mrisho Kikwete ambacho kimetokea nchini India.

Tupo pamoja na familia kwenye kipindi hiki kigumu. Kifo cha mzee wetu huyu kimetugusa sana, maana alikuwa kada mtiifu wa CCM na taifa kwa ujumla. Kazi ya mola haina makosa, tutaendelea kukumbuka na kukuenzi kwa yale yote mazuri uliyo fanya, kushauri na kuyatenda katika uhai wako. Tunaomba wana familia, ndugu, 

 
jamaa, marafiki na viongozi wote tuwe wavumilivu katika wakati huu wa majonzi na huzuni. Lakini tunawashukuru madaktari na wauguzi ambao walijitahidi kuokoa uhai wake.

Inna lillahi wainna ilayhi rajiuun.
Mungu amlaze mahala pema peponi. Amina.

Zainab Abdallah,
M/kiti Shirikisho Taifa.

No comments:

Post a Comment