Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, October 25, 2016

MAHAKAMA YA RUFAA YASHIDWA KUTOA UKUMU KESI YA UCHAGUZI INAYOWAKIBILI ONESMO NANGOLE NA DKT KIRUSWA

mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiongea na waandishi wa habari mara baada ya  maamuzi ya ruf
aa iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la longine Onesmo Nangole
Na Woinde Shizza,Arusha 

Mahakama ya rufaa kanda ya Arusha imeshindwa kutoa maamuzi ya rufaa iliyofunguliwa  na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido ,Onesmo Nangole(CHADEMA) ambaye anapinga maamuzi ya mahakama kuu iliyomvua ubunge wake, badala yake imeagiza mwanasheria mkuu wa serikali na msimamizi mkuu wa uchaguzi katika jimbo hilo aunganishwe katika shauri hilo.

Aidha mahakama hiyo imetoa siku 21 kwa mrufani kwa ajili ya kufanya marekebisho ya notisi yake ya rufaa na kuyaleta mahakamani hapo ili msimamizi wa uchaguzi pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali waingizwe  kama mashaidi  muhimu katika rufaa.

Akisoma taarifa ya majaji watatu walikuwa wakisikiliza rufaa hiyo mahakamani hapo Msajili wa mahakama rufaa John Kayanza alisema kuwa mahakama ya rufaa aitatenda haki katika hukumu yake iwapo haita msikiliza mwanasheria wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Longido na imewataja kama mashaidi muhimu kwa upande wa mrufani


“kama mahakama itatoa uamuzi bila kusikiliza mwanasheria wa serikali na msimamizi wa uchaguzi haitakuwa imetenda haki  katika mahamuzi hivyo mahakama imeonelea ni vizuri  mrifani akaifanyie marekebisho notisi yake na ndani ya siku 21 aiwasilishe mahakamani”alisema Kayanza

Katika rufaa hiyo mrufani Onesmo Nangole aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido alikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu kanda ya Arusha ambayo ilitengua ubunge wake na kuagiza msimamizi  wa uchaguzi atangaze jimbo hilo kuwa lipo wazi.

Katika kesi hiyo Onesmo Nangole( CHADEMA) anawakilishwa na mawakili wawili ambao ni  Methodi kimomogoro akisaidia na wakili John Materu ambapo kwa upande wa warufaniwa Dkt.Steven Kiruswa (CCM) anawakilishwa na mawakili watatu wakiongozwa na DKT.Masumbuko Lamwai akisaidiwa na Daudi Haraka pamoja na Edmond Ngemela.

Rufaa  hiyo inasikilizwa  na Majaji  watatu ambao ni jaji Sauda   Mjasiri,Jaji Musa Kipenka pamoja na Profesa Ibrahimu Juma.

Akiongea mara baada ya kesi hiyo kuairishwa Onesmo Nangole alisema kuwa anaishukuru mahakama kwa kuwapa nafasi na kuona umuimu wa mwanasheria wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wilayani longodo kuja kutoa ushaidi katika shauri hilo na anaamini mahakama hiyo itamtendea haki.


Kwa upande wa Dkt,Kiruswa (CCM) alisema yeye atatizo na maamuzi ya mahakama na anaiachia mahakama iendelee kushulikia shauri hilo na anaamini itatenda haki.

No comments:

Post a Comment