TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Abdulrahman Kinana ameitumia
salamu za rambirambi familia ya Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Iringa
Mzee Tasili Mung’wenya Mgoda aliyefariki dunia jana tarehe 14 Oktoba,
2016 katika Hospitali ya Wilaya ya Mafinga.
Mzee
Mgoda amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya TANU baadae
CCM na Serikalini ambapo amekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Mafinga,
Katibu wa CCM ngazi ya Wilaya na Mkuu wa Wilaya Mstaafu.
Katika
Salamu hizo Ndg Kinana amesema amepokea kwa majonzi na masikitiko
makubwa kifo cha Mzee Tasili Mgoda ambaye alikuwa ni sehemu ya hazina ya
wazee wa CCM na kwamba anaungana na familia ya marehemu, ndugu na jamaa
katika kipindi hiki kigumu cha huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao.
WanaCCM tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mzee Tasili Mung’wenya Mgoda. Amina
Imetolewa na:-
SELEMAN Y. MWENDA
Kny: MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
15/10/2016
No comments:
Post a Comment