Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akitia saini katika Kitabu cha maombolezo cha Harith Mwapachu,
ambaye ni mtoto wa Juma Mwapachu, aliyefariki dunia jana asubuhi.Kulia
ni Balozi Juma Mwapachu. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Freeman Mbowe,
wakati walipokutana katika msiba wa mtoto wa Balozi Juma Mwapachu,
Harith Mwapachu nyumbani kwa Mwapachu Mikocheni jijini Dar es Salaam
jana Oktoba 11. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waombolezaji, wakati akiondoka nyumbani kwa Balozi Juma Mwapachu, wakati alipofika kutoa pole kufuatia kifo cha mtoto wa Balozi Juma Mwapachu, Harith Mwapachu jana Oktoba 11. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na mke wa Balozi Juma Mwapachu, Rose Mwapachu,
wakati alipofika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam jana
jioni kumpa pole kufuatia kifo cha mtoto wake, Harith Mwapachu
kilichotokea jana asubuhi, Oktoba 11, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment