Mabingwa
watetezi wa kombe la mataifa bingwa barani Afrika, Chipolopolo ya
Zambia, leo wamebaunduliwa nje ya mashindano ya kuwania kombe la mataifa
bingwa barani Afrika baada ya kutoka sare 0-0 na Burkina Faso katika
mechi yao ya mwisho ya makundi.
Burkina
Faso imeanza mechi hiyo kwa bahati mbaya baada ya nyota wake Alain
Traore kupata jeraha na kuondolewa uwanjani baada ya dakika kumi pekee.
Traore amefunga magoli matatu zikiwemo mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Ethiopia ambayo walishinda kwa magoli manne ya yai.
Dakika
chache baadaye Davis Nkausu, wa Zambia vile vile alijeruhiwa na
kuondolewa uwanjani na mahala pake kuchukuliwa na Joseph Musonda baadda
ya kugongana na mlinda lango wa Burkina Faso.
Kufikia wakati wa mapunziko timu hizo mbili zilikuwa zimetoshana nguvu ya kutofangana bao lolote.
katika kipindi cha pili Zambia ilifanya mashambulio kadhaa katika lango la Burkina Faso, lakini juhudi zao zligonga mwamba.
Mechi
hiyo ilimalizika huku timu hizo mbili zikigawamna alama moja kila moja
na hivyo Burkina Faso kusonga mbele baada ya kukusanya jumla ya alama
tano nayo zambia ikiridhika la alama mbili.
Nigeria imeongoza kundi hilo kwa jumla ya alama tano huku Ethiopia ikivuta mkia na alama moja.
No comments:
Post a Comment