Akihojiwa na televisheni ya Marekani, CBS, Bwana Assad alisema ikiwa serikali ya Rais Obama ina ushahidi kuwa alihusika, basi iutoe.
Rais Assad aliongeza kuwa washirika wa Syria watajibu shambulio lolote litalofanywa dhidi yake.(P.
Mwandishi wa BBC mjini Washington
anasema Rais Assad amechagua wakati muwafaka kwa mahojiano hayo, kwa
sababu punde baraza la congress litaanza kujadili azimio kuidhinisha
Marekani kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya Syria.
Awali Jumapili mjini Paris Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, alisema mawaziri wenzake wa Jumuia ya Kiarabu walikubali kuwa ikiwa Syria ilitumia silaha za kemikali, basi ilipindukia viwango vya kimataifa.

No comments:
Post a Comment