Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akisalimiana
na baadhi ya wakazi wa Gongo la Mboto mara baada ya kuwasili kiwanda
cha KIKUTA
Diwani wa
Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza machache kabla ya kumkaribisha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa
kuznugmza na wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto.
Mh. Dkt.
Huvisa amempongeza Diwani wa Kata hiyo ambaye pia ni Meya wa Halamshauri
ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwa jitihada zake za kuhamasisha usafi
kwenye Manispaa yake na kuzitaka Manispaa zingine kuiga mfano wa
Manispaa ya Ilala ambapo pia amewahamasisha wakazi wa Gongo la Mboto
kutunza Mazingira kwa kupanda miti ili kukabiliana na manadiliko ya
tabianchi yanayopelekea ongezeko la Joto duniani.
Mh. Dkt.
Terezya Huvisa akiangalia maji ya michoro iliyopo katika kiwanda hicho
inayohamasisha suala utunzaji wa Mazingira majumbani.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akipata
maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi kiwanda hapo namna
wanavyotengeza Mbolea kwa kutumia taka zilizooza.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akingalia
Mbolea iliyozalishwa kiwanda hapo tayari kwa matumizi.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akikagua
kifaa kinachotumika kuchambulia taka kwa ajili ya kuzalishwa upya
kiwandani hapo.
Mratibu
wa Jamii na miradi kutoka Bremen Overseas Research and Development Bi.
Larissa Duma (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (katikati) alipotembelea na
kukagua kiwanda cha KIKUTA. Kushoto ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto
na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya
Huvisa kwenye picha ya pamoja na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye
pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja wa
wafanyakazi wa kiwanda cha kuchambua taka (KIKUTA).
Manispaa ya
Ilala katika Kata ya Gongo la Mboto imezindua kiwanda cha kuchambua taka
chenye uwezo wa kutengeneza Mbolea, Mboji na bidhaa mbalimbali
zitokanazo na taka ngumu na nyepesi.
Kiwanda hicho awa kilijulikana kama kituo
cha kutupia taka (KIKUTA) ambacho kilijengwa na mfadhili Bremen Overseas
Research and Development kutoka Canada.
Kiwanda hicho cha kipekee kimetokana
na juhudi za wakazi wa Gongo la Mboto na Kikundi cha Gongo la Mboto
Youth Group wakisaidiana na viongozi wao na Diwani wa Kata ya Gongo la
Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry
Silaa.Kiwanda hicho kitatoa ajira kwa vijana ili kujikwamua kwenye lindi la umaskini.
No comments:
Post a Comment