Sakata la kusambaa picha zisizokuwa na maadili mitandaoni
zikiwemo za watu maarufu hapa nchini leo limezungumziwa tena katika bunge la
Tanzania kule Dodoma ambapo katika kipindi cha maswali na
majibu Mhe. Habib Mnyaa ameonekana akihoji serikali
inachukua hatua gani juu ya watu wanaotuma picha zao zisizo na maadili
mitandani zikiwemo za kina Wema na Diamond wanazopiga wakiwa chumbani na kuweka
kwenye mitandao.Katika majibu yake waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia
Prof. Makame Mbarawa anasema “Mhe. Spika kuhusu picha zisizokuwa na maadili
zinazowekwa katika mitandao na watu maarufu na hata wasiokuwa maarufu serikali
imeanza kuandaa kanuni zitakazokuwa zikifuatilia Online Content ambapo itaanza
kuchukua hatua baada ya kufuatilia juu ya picha hizo na kuchukua hatua
madhubuti”.
Baada ya kauli hiyo Spika wa bunge Mhe. Anne Makinda
alikazia akitaka majibu juu ya picha za juzi zilizosambaa zikimuonyesha Mhe.
Komba akiwa na binti mdogo ambazo mwenyewe alisema si zake na wabunge kuonekana
wakitaka majibu ambapo Mhe. Mbarawa anasema.
“Mhe. Spika kuhusu picha za juzi zilizosambaa mitandaoni
tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata mimi bado
sijaziona ila tutachukua hatua tutakapobaini zilipotoka
No comments:
Post a Comment