Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko kubwa
la ardhi mashariki mwa Uturuki imefikia takriban watu mia mbili huku
wengine wengi wakiwa hawajulikani waliko au kujeruhiwa.
Tetemeko hilo limekuwa na vipimo vya saba nukta mbili kwenye mizani ya ritcher.
Majeruhi na maafa yameripotiwa hasa katika mji wa Ercis ambako majengo thelathini yaliporomoka. Mji ulio karibu wa Van nao pia uliathirika vibaya sana.
Harakati za uokoaji zimeendelea usiku kucha.
No comments:
Post a Comment