Katibu Mkuu wa Chama cha mpira wa miguu Poland PZPN,
Zdzislaw Krecina katika picha.
Chama cha Mpira wa Miguu Poland (PZPN)
kimetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa
ajili ya mchezaji Khatib Waziri Mzee ili aweze kucheza mpira wa miguu
nchini humo.
PZPN imetuma maombi
hayo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kumwezesha
mchezaji huyo kuichezea timu ya LUKS Wierzbiecice ambayo hata hivyo
haikuelezwa iko ligi ya daraja gani nchini humo.
Kwa mujibu wa Katibu
Mkuu wa PZPN, Zdzislaw Krecina, Mtanzania huyo aliyezaliwa Julai 30,
1974 ameombewa hati hiyo kama mchezaji wa ridhaa kwa maelezo kuwa
hakuwahi kusajiliwa na klabu yoyote nchini.
TFF inafanyia kazi
maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya taratibu husika
kukamilika.
No comments:
Post a Comment