Kiungo wa timu ya Coastal Union, Sabri Ramadhan ‘China’ amechaguliwa
kuwa mchezaji bora wa mwezi Septemba katika Ligi Kuu ya Vodacom.
China
alichaguliwa kutokana na kupata pointi nyingi kwenye mechi alizocheza
kwa mwezi huo. Baadhi ya mechi alizopata pointi nyingi ni dhidi ya
African Lyon na JKT Ruvu Stars.
Katika mechi namba 27 dhidi ya
Lyon iliyochezwa Septemba Mosi kwenye Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es
Salaam na timu yake kushinda bao 1-0 alipata pointi 85 kati ya 100.
Vilevile
alipata pointi 89 kwenye mechi namba 33 dhidi ya JKT Ruvu Stars
iliyochezwa Septemba 5 mwaka huu Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.
Coastal Union ilipoteza mechi hiyo kwa mabao 3-0.
Kwa kuibuka
mchezaji bora wa Septemba, China atazawadiwa kitita cha sh. 600,000
kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom
Mchezaji
bora wa Agosti alikuwa kiungo wa Polisi Dodoma, Ibrahim Massawe ambaye
kwenye mechi namba 4 ya ligi hiyo dhidi ya African Lyon iliyochezwa
Agosti 20 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma alipata pointi 93
ambazo hazikufikiwa na mchezaji yeyote kwa Agosti.
MCHEZAJI
AOMBEWA ITC POLAND
Chama cha Mpira wa Miguu Poland (PZPN) kimetuma
maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya
mchezaji Khatib Waziri Mzee ili aweze kucheza mpira wa miguu nchini
humo.
PZPN imetuma maombi hayo Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) ili kumwezesha mchezaji huyo kuichezea timu ya LUKS
Wierzbiecice ambayo hata hivyo haikuelezwa iko ligi ya daraja gani
nchini humo.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa PZPN, Zdzislaw Krecina,
Mtanzania huyo aliyezaliwa Julai 30, 1974 ameombewa hati hiyo kama
mchezaji wa ridhaa kwa maelezo kuwa hakuwahi kusajiliwa na klabu yoyote
nchini.
TFF inafanyia kazi maombi hayo na hati hiyo itatolewa
mara baada ya taratibu husika kukamilika.
LIGI KUU YA VODACOM
Mechi
za wiki hii za Ligi Kuu ya Vodacom ni kama ifuatavyo;
Oktoba 24-
Coastal Union vs Polisi Dodoma (Uwanja wa Mkwakwani)
Oktoba 24-
African Lyon vs Villa Squad (Uwanja wa Chamazi)
Oktoba 25- Moro
United vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Chamazi)
Oktoba 25- Mtibwa Sugar
vs Azam (Uwanja wa Manungu)
Oktoba 26- Toto Africans vs Kagera Sugar
(Uwanja wa CCM Kirumba)
Oktoba 28- JKT Ruvu vs African Lyon (Uwanja
wa Chamazi)
Oktoba 29- Yanga vs Simba (Uwanja wa Taifa)
Oktoba 29-
Polisi Dodoma vs Oljoro (Uwanja wa Jamhuri)
Oktoba 29- Toto Africans
vs Coastal Union (Uwanja wa CCM Kirumba)
Oktoba 30- Kagera Sugar vs
Azam (Uwanja wa Kaitaba)
Oktoba 30- Villa Squad vs Ruvu Shooting
(Uwanja wa Chamazi)
Oktoba 30- Mtibwa Sugar vs Moro United (Uwanja wa
Manungu)
MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI
Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa na mkutano na waandishi wa habari
utakaofanyika kesho (Oktoba 24 mwaka huu)
Muda: Saa 6.00
Mahali:
TFF
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment