Tofauti na wasanii wengi duniani, Rapa 50 cent ameamplfy kuhusu sababu za yeye kutotumia vilevi kama dawa za kulevya na pombe, vilevi ambavyo vinatumiwa na wasanii wengi sana duniani hata wanapokua kwenye STAGE.
50 amesema ni kutokana na kuwahi kushuhudia watu wake wa karibu kama vile ndugu zake wakitumia vilevi kwa time tofauti na waliishia kuharibikiwa kiafya na kimaisha kwa ujumla.
Pamoja na kwamba ulimwengu mzima unafahamu kwamba 50 cent aliwah kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, lakini hakuwah kutumia dawa hizo hata siku moja.
Hata hivyo amekiri kwamba amewah kutumia pombe, na kusema kwamba ulevi uliwah kumfanya aharibikiwe kisaikolojia, kama kupata uoga na msongo wa mawazo lakini baada ya kugundua pombe ndio sababu ya hayo matatizo, aliamua kuachana nayo.

hii
ni moja ya MAJUMBA ya Kifahari yanayomilikiwa na 50 CENT, aliinunua
kutoka kwa MIKE TYSON, na anaamini ameweza kufanya mambo mengi ya akili
kwa sababu ni timam kwa sababu hajihusishi na ulevi kama dawa za kulevya
ambazo zimeharibu maisha ya wasanii wengi ambao mpaka leo hawakutumia
mkwanja wao vizuri kufanya mambo ya maana, kama YOUNG BUCK member wa
zamani wa G UNIT, mfano mzuri kwa LANGA pia wa Bongo, ambae baada ya
kugundua dawa za kulevya ni soo ameamua kuziacha, bado akijutia muda
alioupoteza
No comments:
Post a Comment