ARUSHA TECHNICAL COLLEGE YA SAINI MAKUBALIANO YA USHIRIANO (MoU) NA TAASISI YA PUM YA NCHINI UHOLAZI
Na: Gasto Leseiyo
Chuo
cha Ufundi Arusha (ATC) kimesaini Makubaliano ya Ushirikano (MoU) na
Taasisi ya PUM ya chini Uholazi kwa lengo la kuongeza ujuzi kwa
wakufunzi wanaofundisha programu za Uhandisi Umeme pamoja na Uhandisi Elekroniki na Mawasiliano Anga
Katika
makubaliano hayo, Taasisi ya PUM itaisaidia ATC itatoa Wataalamu
mbalimbali katika fani za Umeme na Electroniki na Mawasiliano Anga ili
kujenga Ujuzi na Umahiri kwa Wakufunzi wa ATC.
Awali
akizungumza mara baada ya kusaini Makubaliano ya Ushirikano, Mkuu wa
Chuo cha Ufundi Arusdha, Mhandisi. Dkt. Richard Masika alisema kuwa, kwa
sasa ujuzi na umahiri unaohitajika katika viwanda vingi nchini
hauendani na kile Wahitimu nwengi wa fani za ufundi wanakitoa hali iliyopekea kushirikiana na Taasisi ya PUM ya nchini Uholazi kwa lengo la kuongeza na kujenga Ujuzi na Umahari kwenye mafunzo kwa vitendo.
Aliendelea kusema kuwa, mradi huu wa PUM sio tu tutasaidia kuongeza Ujuzi zaidi kwa Wakufunzi bali pia kusaidia kujenga ushiriano na viwanda na Taasisi mbalimbali hapa nchini zinazoajiri wahitimu chuo cha Ufundi Arusha.
“Mradi
huo wa PUM na Chuo cha Ufundi Arusha umelenga kuunda Mtahala na vyenzo
mbalimbali za kufundishia pamoja na kutambua vifaa mbalimbali vya
kufundishia vinayohitajika katika kwenye mafunzo ya vitendo. Pia umelenga kuongeza ushirikano na viwanda, Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Chuo chetu cha Ufundi Arusha ” alisema Dkt. Masika
Awalia
akizungumza wa Wadau mbalimbali wa Ufundi Chuoni hapao, Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya PUM, Bw. Thijs Van Praag alitoa changamoto kwa
uongozi wa Chuo, kufanya utafiti kwa wahitimu wote wanaomaliza Chuoni hapo wanachukua muda kiasi hadi kupata ajira au kujiajiri wenyewe katika fani walizosemea.
“Kama
wanafunzi inawachukua miezi sita au mwaka moja kupata ajira au
kujiari, hii inamanisha kuwa kile kinachofundishwa akiendani na
mahitaji ya soko na kama hivyo ndivyo, itakuwa ni jambo la busara
kuangalia tena mitahala inayotumika na kuakikisha kuwa progaramu
zinazofundishwa zina msaidia mwanafunzi na jamii kwa ujumla” alisema Bw. Praag
No comments:
Post a Comment