HATARI ILIYO MBELE KWA WAMACHINGA WANAOONGEZEKA KWA KASI KATIKA MATAA YA UBUNGO SERIKALI MNAIONA?
Kwa
kipindi kirefu sasa eneo la Ubungo karibu na Mataa ya kuongozea magari
yanayo ingia Jijini au yale yanayotoka pande mbili, mengine yakitokea
Mwenge na mengine yakitoke Buguruni na kwenda sehemu mbali mbali za
jiji limevamiwa na wafanya biashara ndogo ndogo maarufu kama
Wamachinga.
Nimejaribu
kulifuatilia kwa kipindi kirefu ili kuweza kujiridhisha kujua kama
wamepewa ruhusa na nani kufanya biashara katika eneo lisilo rasmi,
nilijaribu kuongea na wamachinga wachache; wa kwanza anaitwa Salum
Ramadhan anauza taa za kichina katika eneo hilo, yeye alidai
hawajaruhusiwa na mtu kufanya biashara hapo ila ni kutokana na ugumu wa
maisha ndio umewapelekea kufanya biashara katika eneo hilo na wa pili
naye Ndg. Deogratius Shirima akasema maneno hayo hayo ambayo
hayapishani maana na huyu wa kwanza.
Sikuishia
hapo nikataka kujua je kuna mtu yeyote ambaye anakuja kukusanya japo
ushuru kutoka kwao? nao kwa pamoja wakasema kuna mtu huwa anakuja
kukusanya ushuru lakini wao hawana uhakika kama ni kutoka Serikali za
mitaa au la! nikawauliza swali jingine, huyu jamaa ambaye ameweka
jenereta hapa na kuwapa huduma ya Umeme mnamlipa Sh. ngapi? wakasema
kila taa 1 ni Sh. 1000/- nikapenda nijue sasa swali langu la msingi,
wanajua HATARI iliyo
mbele yao kutokana na kufanya biashara kando kando ya bara bara kubwa
kama hii ambayo inapitisha magari mengi na hasa mengine yanakuwa yako
kwenye mwendo wa kasi! wakasema wanaifahamu ila hawana jinsi wataenda
wapi na maisha yenyewe ni magumu!
Kwa kweli nilitoka bila kuwa na jibu sahihi nini hatma yao kama gafla gari likitoka kwenye bara bara na kuwavama.
Tatizo
hili naamini serikali wanaliona ila wanalifumbia macho na pindi ajali
itakapo tokea ndio wanafumbua macho na kujua sehemu sio halali, ni vema
serikali ikalichukulia hatua mapema kabla halija tokea la kutokea.
Tumekua tukiona sehemu mbali mbali ajali zinatokea na kuua watu wengi
ambao wapo kando kando ya bara bara kwa hiyo ni vema Serikali ikachukua
tahadhari mapema.
No comments:
Post a Comment