Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 3, 2011

CHELSEA: hatujafurahishwa na mashabiki kumzomea ANTON FERDINAND


Club ya soka ya Chelsea imekemea kelele ambazo zimekua  zikisikika kutoka kwa mashabiki wa club hiyo dhidi ya beki wa qpr Anthony Ferdinand wakati wa mchezo kati ya Chelsea na GENK Jana.

Mashabiki waliosafiri kutoka England mpaka ubelgiji, walikua wakiimba nyimbo za kumkashifu antorn Ferdinand ambae inasemekana alitolewa maneno ya kibaguzi na mchezaji wa Chelsea John terry wiki iliyopita.

Msemaji wa Chelsea amesema kwamba hawajafurahishwa na kilichofanywa na mashabiki hao na kama club hawataki ziendelee.


kocha wa chelsea Andre Villa Boas.

hata hivyo Kocha wa Chelsea andre villa boas amejiweka pembeni, kwa kusema hana chochote cha kusema kuhusiana na walichokua wanaimba mashabiki wa Chelsea jana.

jana mashabiki wa Chelsea, walikua wanaimba kwa kusema anton Ferdinand unajijua wewe ni nani.

Na ilionekana kama wanazidi kukitonesha kidonda, kwa sababu tusi zito alilotukanwa na john terry lilisema wewe ni…… wa afrika…. neno zito limefichwa kwenye desh, sasa jana mashabiki wa Chelsea ndio walikua wanaiwekea chumvi hiyo kauli.

No comments:

Post a Comment