mbunge wa kigoma kaskazini, Zitto Kabwe amefanyiwa opareshen ya
KIPANDAUSO leo, opareshen ambayo imedumu kwa saa nne kwenye hospitali ya
Apollo, Bangalore -India.
hali ya sasa ya mbunge huyo ni nzuri, na kwa mujibu wa maelezo ya
kaka yake ambae wako pamoja, ni kwamba wanatarajiwa kuruhusiwa kutoka
hospitali siku tatu zijazo.
Salum amesema bado wako hospitali, na kwamba sasa hivi mbunge huyo
japokua hawezi kuzungumza sana, amesema kichwa kilichomsumbua sana toka
wiki iliyopita, hakimuumi tena, na pia damu hazitoki.

hii ni moja ya muonekano wa ndani wa hospitali ya Apollo - Bangalore.
Zitto Kabwe alisafirishwa ijumaa iliyopita kwenda India baada ya kugundulika kwamba hakukuwa na uwezekano wa kutibiwa bongo.
kuumwa kwa Zitto kulifanya baadhi ya taarifa za kupotosha kuenezwa kwa kasi kwamba mbunge huyo amefariki dunia.
hata hivyo hali yake imebadilika sio kama wiki iliyopita, ambapo juzi
kwa mara ya kwanza, alipata nafasi ya kuzungumza na mashabiki zake
kupitia kurasa zake za fB na twitter, na kuamplfy kwamba anaendelea
vizuri, hivyo wasiwe na hofu yoyote
No comments:
Post a Comment