Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 3, 2011

HOTNEWS....WANAFUNZI WAMCHARAZA BAKORA MKUU WA SHULE BAADA YA KUGOMA KUVUJISHA PEPA....

HOTNEWS....WANAFUNZI WAMCHARAZA BAKORA MKUU WA SHULE BAADA YA KUGOMA KUVUJISHA PEPA....



HAKIKA ukistaajabu ya Mussa utayaona ya filauni katika hali isiyotegemewa na walimu wa shule ya sekondari ya Ikola mkoani Rukwa ni baada ya wanafunzi kugeuka mbogo kwa walimu wao kwa kuamua kumcharaza bakora kwa niaba ya walimu wengine mkuu wa shule hiyo ambaye aligoma kushawishi walimu wenzake kuvujisha mtihani ili waweze kutafuta majibu kabla ya kuingia chumba cha mitihani.

Kutokana na hali hiyo jeshi la polisi mkoani Rukwa linawashikilia viongozi wa wanafunzi hao waliojitoa mhanga kumcharaza bakora mwalimu huyo kwa kuwakamata wanafunzi watatu wa kidato cha pili wa shule ya sekondari Ikola tarafa ya Karema kwa tuhuma ya kumshambulia na kumjeruhi mkuu wa shule, baada ya Mwalimu huyo kukataa kushinikizwa na wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ili kuvujisha mtihani wa kidato cha nne uliofanyika hivi karibuni shuleni hapo.

Mwandishi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Sumbawanga Elizabeth Ntambala anaripoti kuwa Kamanda wa polisi mkoani Rukwa.Isuto Mantage alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tano asubuhi wanafunzi hao waliokuwa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha tatu walifanya vurugu hizo baada ya kuwafungia walimu wengine kwenye ofisi yao kisha kwenda kuvamia ofisi ya mkuu wa shuile hiyo Kateka Chipeta.

Mantage alidai kuwa wanafunzi hao walifanikiwa kuwashawishi wenzao takribabi 260 na kwenda kuvamia ofisi ya mkuu wa shule na kuanza kumpiga kwa fimbo na mangumi kabla ya Chipeta kufanikiwa kupokonyoka na kwenda kujisalimisha kwenye ofisi ya Mtendaji wa kata hiyo.

Inadaiwa kuwa kufuatia kipigo hicho ilibidi Mkuu wa shule akimbizwe katika zahanati ya kijiji hicho ambako alitibiwa na baadaye kuruhusiwa baada ya kupata michubuko kwenye maeneo mbalimbali ya mwili.

Uchunguzi uliofanywa awali umebaini kuwa wanafunzi hao waliamua kufanya vurugu hizo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wenzao wa kidato cha nne juu ya kushindika kwa mpango wao wa kumshawishi mkuu wa shule hiyo kupokea fedha walizochanga ili amshawishi msimamizi wa mitihani ya kidato cha nne kwa lengo kuvujisha mitihani hiyo.

“Hawa wanafunzi wanadaiwa kuwa walichanga fedha na kumpatia mkuu wa shule yao ili ampatie huyo msimamizi lakini Mkuu wa shule hiyo alikataa kufanya kitendo hicho cha uvunjaji wa sheria hali iliwaudhi wanafunzi hao kiasi cha kulazimika kuwaeleza wenzao wa madarasa ya chini yao walioamua kumpia mkuu wao wa shule” Alisema Mantage.

Kufuatia uchunguzi wa habari hizi ulibaini kuwa pia wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakichangishwa fedha kwaajili ya kuchangia gharama za kuwalipa posho Walimu wa kujitolea wanaofundisha shuleni hapo kutokana na shule hiyo kuwa na Walimu wawili pekee.

Akizungumza kwa simu kutoka Ikola Patrick Charles alisema kuwa mara nyingi michango hiyo imekuwa ikifanyika na wazazi wamekuwa wakitoa ili watoto wao waweze kupata elimu lakini katika siku za karibuni wanfunzi wamekuwa wakilalamika kuwa hawafundishwi kwani hata hao walimu wakujitolea wamekuwa hawafiki shuleni hapo na kuongeza kuwa ndio cha chanzo cha vurugu.

“Baada ya kuona Walimu hao wakujitolea hawaji na wamekuwa hawasomi walimwuliza mkuu wa shule ambaye alishindwa kuwajibu majibu yaliyotii kiu yao na ndio chanzo kikubwa cha vurugu hizo kutokea” Alisema Patrick.

No comments:

Post a Comment