Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, November 6, 2011

MADEREVA WA MAGARI YA ABIRIA WAANZISHIWA BIMA

MADEREVA WA MAGARI YA ABIRIA WAANZISHIWA BIMA

Na Mashaka Baltazar ,MWANZA
KAMPUNI ya Jubilee Insurance Ltd imeanzisha huduma mpya ya bima ya vikundi kwa madereva , itakayowezesha kwenda sambamba na utoaji wa bima ili kuwasaidia kupata kinga pindi wanapopata matatizo ya ajali kazini.
Kwamba hadi sasa madereva 50 wa Kanda ya Ziwa wamejiunga na huduma hiyo ambayo imeanzishwa na kampuni hiyo yenye makao yake Jijini Nairobi Kenya .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hivi karibuni mara baada ya semina elekezi kwa baadhi ya madereva wa Kanda ya Ziwa, Meneja Mikopo wa Jubilee Insurance, Willson Mnzava, alisema kuanzishwa kwa huduma ya bima kwa vikundi kutawanufasiha madereva hao ambao ni kundi lililosahaulika kati ya makundi yanayopata huduma za bima.
Mnzava , alisema manufaa wakayoyapata endapo watajiunga na bima hiyo ya vikundi ni pamoja na malipo ya ajali na vifo wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao .
Alisema wamefikia kuanzisha huduma ya bima kwa vikundi baada ya kubaini kwamba kati ya bidhaa zote za bima zinazotolewa , kundi la madereva na makondakta limesaulika kwani huduma za bima hasa kwa magari ya abiria, zinawatambua abiria na magari pekee na kuliacha kundi hilo.
‘‘ Katika bima zote zilizopo kwenye magari zinawatambua abiria na gari lenyewe, lakini madereva wamesahulika, Jubilee Insurance kwa kuliona hilo tumeanzisha bidhaa mpya kwa madereva ambayo itakuwa msaada kwao katika kupata haki pindi linapotokea tatizo la ajali,”alisema Mnzava.
Alisema kima cha chini kitakachotozwa katika bima hiyo kwa dereva kila mwezi kwa kundi la kwanza ni shilingi 5,000 , ambapo kundi la pili kiwango kitakachotozwa ni shilingi 7,000.Hivyo kila dereva atachagua ni kundi lipi atajiunga nalo kutokana na kuwapo makundi mawili.
Alieleza kwamba endapo dereva atafariki au kupata janga lolote atalipwa kuanzia shilingi milioni 1,500,000 hadi milioni 7,000,0000, na kuwataka mdereva kuchangamkia huduma hiyo ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwao.
Aidha Mwenyekiti wa chama cha Madereva Kanda ya Ziwa, Dede Petro kampuni hiyo ya bima wazo la kuanzishwa kwa huduma hiyo kwa madereva limekuja wakati muafaka na kilio chao kimesika
“Niwashukuru Jubilee Insurance kwa kuanzisha bidhaa hii mpya kwa madereva na makondakta baada ya kuona umuhimu wao katika jamii, kwetu sisi madereva hitaji hilo lilikuwa ni changamoto kubwa,sasa tumefarijika baada ya kilio chetu kusikika,” alisema Petro.
Alisema tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo ya bima kwa vikundi madereva 50 wamejiungajambo linalodhihirisha kuwa kadri siku zinavyokwenda wengi wa madereva watajiunga na bidhaa hiyo nzuri ambayo imeanzishwa mahususi kwa ajili yao.

No comments:

Post a Comment