Mheshimiwa Nchimbi mgeni rasmi uzinduzi wa Albamu ya Anti Virus 2
Gradice Sigera
Maelezo
Dar es Salaam
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo
Dkt.Emanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa
albamu ya wanamuziki wa kizazi kipya inayoitwa Anti Virus 2.
Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam
mratibu wa uzinduzi huo ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph
Mbilinyi alisema uzinduzi wa albamu hiyo unalengo la kuwakomboa vijana
waweze kunufaika na kazi zao.
Mheshimiwa Mbilinyi amesema kwa muda mrefu
wasanii wa muziki wa kizazi kipya wamekuwa wakizulumiwa na wajanja
wachache kitu ambacho kimewaacha wasanii hao kuendelea kuwa maskini.
"Kuna wajanja wachache ambao kwa muda wa miaka mingi
wamekuwa wakinufaika na jasho la wasanii sasa tumeamua kufanya
mapinduzi kwa kuwaungunisha wasanii ili waweze kutetea haki
zao".Alisema Mheshimiwa Mbilinyi.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika
viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii tarehe 26 Novemba kuanzia saa 12-6
usiku ambapo jumla ya wasanii zaidi ya 20 watashiriki ikiwa ni pamoja
na waheshimiwa wabunge na mawaziri ambapo kiingilio kitakuwa ni
shilingi 5000.
Katika tamasha hilo Mheshimiwa Mbilinyi atauza kitabu kinachoelezea historia ya maisha yake ambacho kitauzwa kwa shilingi 5000.

No comments:
Post a Comment