Lionel Messi alitunukiwa tuzo ya FIFA Ballon d’O kwa mara ya tatu mfululizo.
Barcelona;s
24-year old Argentina striker aliwashinda mchezaji mwenzie wa Barcelona
Xavi na mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo katika tuzo hiyo
ya mchezaji bora wa mwaka.
Shemejiiiiiiiii Shakira akimpongeza Lionel Messi.
Messi,
man of the match katika champions league final mwaka 2011, pia
alishinda kombe la La Liga, Spanish Supercopa, UEFA Super Cup na Kombe
la klabu bingwa ya dunia mwaka uliopita.
Manager wa Manchester United Sir Alex Ferguson na Xavi wote walitoa maneno ya heshima kwa Messi.
Ferguson
alisema Messi anaweza kuwekwa katika mizani ya magwiji wa soka duniani
katika miaka mingi ijayo, hata kama bado ana miaka 24.
‘Maneno
yamekuwa yakisemwa kila kuhusu kwamba wachezaji kama Pele kutoka katika
zama za miaka ya 50 wangeweza kucheza katika kipindi hiki, jibu ni
kwamba wachezaji wakubwa wanaweza kucheza katika kizazi chochote. Lionel
Messi angeweza kucheza katika miaka ya 1950s na sasa pia, kama ilivyo
kwa Di Stefano, Pele, Maradona, Cruyff kwa sababu wote ni wachezaji
magwiji.” –Fergie
Messi akipongezwa na washindi wa zamani wa tuzo hiyo Micheal Platini na Ronaldo De Lima,
Xavi
nae alimuunga mkono Ferguson kwa kusema:” Lionel bado mdogo, ana miaka
24 tu na nafikiri atavunja rekodi zote zilizopo katika huu mchezo.
Atakuja kuwa moja ya wachezaji wakubwa waliowahi kutokea katika mchezo
huu wa mpira wa miguu.”
Mapema jioni ya jana Ferguson na Pep Guardiola walizawadia tuzo katika shrehe hizo.
Ferguson alizawadiwa FIFA Presidential award for services to football, na alikabidhiwa tuzo hiyo na raisi wa FIFA Sepp Blatter.
Pep Guardiola alitajwa kama kocha bora wa Dunia in 2011 baaada ya kuiongoza Barcelona kushinda makombe matano
Neymar alishinda tuzo ya Puskas kwa kufunga bao bora la mwaka.
Pia
jana kilitangazwa kikosi bora cha mwaka kwa mujibu wa FIFA huku kikosi
hicho kikitaliwa na wachezaji wa Barcelona, Manchester United na Real
Madrid pekee.
WAYNE ROONEY AKIKABIDHIWA TUZO YA KUWA MOJA YA WACHEZAJI WALIOUNDA KIKOSI CHA MWAKA
KIKOSI CHA FIFA CHA MWAKA
Iker
Casillas (Real Madrid), Dani Alves (Barcelona), Gerard Pique
(Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid), Nemanja Vidic (Man Utd), Andres
Iniesta (Barcelona), Xabi Alonso (Real Madrid), Xavi (Barcelona),
Lionel Messi (Barcelona), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Wayne Rooney
(Man Utd).
No comments:
Post a Comment