Wanafunzi wa chuo cha Mipango (IRDP) -
Dodoma course ya "Finance and Investment" mwaka wa tatu, leo majira ya
saa saba mchana wamevamia kibanda cha mfanyabiashara jirani na chuo
hicho, kwa mujibu wa habari nilizopata ni kwamba wanafunzi hao
walichukua jukumu hilo kutokana na kitendo cha kinyama alichofanyiwa
mwanafunzi mwenzao kwa kupigwa na kujeruhiwa kwa panga kwenye mdomo na
kutolewa jino, kijana huyo ambae ni mfanyabihashara jirani na chuo
anaejulikana kwa jina la Daudi, alimjeruhi mwanafunzi huyo kwa tuhuma za
kumuhisia kuwa anatembea na mkewe, jambo ambalo sio la kweli kabisa kwa
mujibu wa jirani zake wanaojua mpango mzima. Mfanyabihashara huyo
alimfananisha kijana huyo kwa kupewa maelekezo yenye kumlenga mwanafunzi
huyo aliyejulikana kwa jina la Baraka Kajange.
Wanafunzi
hao walichukua jukumu la kukiteketeza kibanda cha mfanyabihashara huyo
baada ya kumkosa mtuhumiwa aliyedaiwa kukimbia mahali hapo. Hata hivyo
uongozi wa chuo kwa kushirikiana na uongozi wa serikali ya mtaa
umeridhia kitendo walichokifanya wanafunzi hao kuwa ni mfano kwa watu
wenye matendo ya kinyama kama mfanyabihashara huyo.
wanafunzi wakikishughulikia kibanda hicho
maezeka ya kibanda hicho yakiwa yametolewa
kibanda kikiwa kimeshusha chote
mabati na maezeka yakiteketezwa kwa moto
Ujumbe toka kwa wanafunzi hao: "huu ni mwanzo ila ataona mwisho,
na kwa wale wenye roho za kinyama kama bwana Daudi waige waone!
"CHEZEA MADENT"
No comments:
Post a Comment