Wimbi
la ajali ya magari ya mizigo/maroli mkoani Mbeya lazidi kutanda,
kutokana na madereva kutochukua tahadhari ya mwendokasi, licha ya mvua
zinazoendelea kunyesha katika msimu huu wa masika. Pichani Askari wa
Kikosi cha Usalama wa barabarani akifanya uchunguzi wa ajali ya tela la
roli lenye nambari ya usajili T 563 AAH na kichwa cha roli aina ya
Scania yenye nambari T 504 ARA, lililokuwa likiendeshwa na dereva Juma
Mombeki kutoka Jijini Mbeya kuelekea Jijini Dar es salaam na kisha
kupinduka Mlimanyoka jijini Mbeya.
Tela la roli lenye nambari ya usajili T 563 AAH na kichwa cha roli
aina ya Scania yenye nambari T 504 ARA, lililokuwa likiendeshwa na
dereva Juma Mombeki kutoka Jijini Mbeya kuelekea Jijini Dar es salaam
na kisha kupinduka Mlimanyoka jijini Mbeya.
Kupishana
kwa magari ya mizigo ndio sababu ya kupinduka kwa tela la roli lenye
nambari ya usajili T 563 AAH na kichwa cha roli aina ya Scania yenye
nambari T 504 ARA, lililokuwa likiendeshwa na dereva Juma Mombeki
kutoka Jijini Mbeya kuelekea Jijini Dar es salaam katika eneo la
Mlimanyoka kama inavyoonesha pichani, roli hilo likipishan ana roli
jingine lenye nambari T 620 AUU lenye tela nambari T 468 AZH lililokuwa
likielekea nchi ya Zambia kutokea Jijini Dar es salaam.
Msongamano
wa magari eneo la Mafiati jijini Mbeya bado halijafanyiwa ufumbuzi,
ikiwa ni pamoja na kuweka taa za barabarani, licha ya kuwepo kwa ajali
za mara kwa mara hasa mida ya jioni. ((Picha naMwandishi wetu .)
No comments:
Post a Comment