Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, March 6, 2012

ANDRE VILLAS-BOAS KWENYE MAZUNGUMZO YA SIRI KUCHUKUA KIBARUA LUISI ENRIQUE ROMA.


Andre Villas-Boas alikutana kwa siri mjini London na mkurugenzi wa AS Roma Franco Baldini mwezi uliopita kuzungumza juu ya mreno huyo kuwa kocha wa klabu hiyo msimu ujao imefahamika.
AVB, ambaye alitimuliwa na Chelsea juzi Jumapili, amekuwa akiwindwa na seria A club kumbadili kocha wa sasa Luis Enrique kipindi kijacho cha kiangazi.
Mtandao wa Goal.com umeweka wazi kwamba mazungumzo katika ya AVB na Baldini yalifanyika katika mgahawa ambao upo karibu na makazi ya Baldini, ambaye aliacha kazi katika timu ya taifa ya England na kujiunga na Roma in October.
Villas-Boas aliulizwa na Baldini kama angekuwa interested kumrithi Enrique, ambaye inasemekana ndio kocha Anayetajwa kumrithi Pep Guardiola akiwa aamua kuhama kocha ataamua kuondoka Nou Camp mwishoni mwa msimu.
Mreno inasemekana alimjibu msaidizi wa zamani wa Capello kwamba alikuwa akihofia kufukuzwa kazi wakati wowote kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya, hivyo alikuwa tayari kuhamia Roma.
Pia Goal.com imefichua kwamba AVB alishakutana na watu  wa AS Roma kabla ya Enrique hajahamia klabuni pale wakati alipokuwa Porto lakini watoto wa PAPA walishindwa dau la kumtoa Porto paundi millioni13.4 ambayo ilikuja kulipwa na Chelsea.
Enrique anaonekana sio mtu wa kufukuzwa Roma – ambayo ni yasita katika msimamo , lakini kuna vishiaria vyote vinavyoonesha kwamba hatakuwepo Italy msimu ujao.
 Chanzo cha habari kutoka kwa Mhispania huyo kinasema kuna makubaliano yam domo kati ya raisi wa Barcelona Sandro Rossell kuchukua nafasi ya Pep ikiwa kocha huyo wa sasa ataamua kuachana na klabu hiyo kwa sasa.
Akiongea baada ya kufungwa katika derby dhidi ya Lazio wikiendi iliyopita, Enrique alisema: “      Kama mpaka sasa siaminiki kama kocha sahihi wa Roma then nitaondoka bila matatizo yoyote
Kwa hisani ya shafih dauda

No comments:

Post a Comment