Newton akisalimiana na Ashley Cole huku John Terry na Di Matteo wakiangalia. |
Chelsea wamejitoa kuwatuliza wachezaji kwa kumleta kipenzi cha klabu hiyo Eddie Newton kuja kuwa kuchukua nafasi katika benchi la ufundi kwa pamoja na mrithi wa muda wa AVB
Roberto Di Matteo.
Mchezaji huyo wa zamani wa The Blues -
ambaye alicheza mechi zaidi ya 200 kwa klabu hiyo aliungana na kikosi
cha sasa leo jumatatu katika uwanja wa mazoezi wa Cobham.
Hii
imekuja masaa 24 baada ya Andre Villas-Boas kutimuliwa na Roman
Abramovich, ambaye sasa anasaka kocha wa 8 katika miaka 9 tangu
alipoinunua timu hiyo.
Marafiki wakweli -tangu wakiwawachezaji mpaka makocha. |
Newton aliambia Sky Sports: “Hii kwa ya The Blues. Lengo ni kuisadia timu angalau kupatanafasi ya nne.
“Kila mchezo ni muhimu kutoka sasa mpaka mwisho wa msimu.”
Aliongeza;
“Siwezi kuongelea kilichokuwa kinatokea kabla, lakini sasa nipo Chelsea
na ninachotaka pamoja na staff wenzangu wote kujitahidi kupata ushindi
katika kila mechi na tutaendelea kufanya mpaka iwe tabia tena.”
Staffs wengine waliomfuata Villas-Boas ni Kocha wa fitness Jose Mario Rocha na skauti wa kufuatiliwa wapinzani Daniel Sousa.
Newton
alijiunga na Chelsea akiwa na miaka 13 na hatimaye alicheza mechi yake
ya kwanza mwaka 1992. Wote wawili Newton na Di Matteo walifunga katika
fainali ya kombe la FA Cup dhidi ya Middlesbrough.
Newton na Di Matteo pia walifanya kazi ya ukocha katika za West Brom na MK Dons.
kwa hisani ya shafih dauda
kwa hisani ya shafih dauda
No comments:
Post a Comment