Waziri
wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar,Mh Ally Mbarouk (kulia) akipena mkono na Mkurugenzi wa Masoko
wa TBL,Kushilla Thomas wakati wakibadilisha mikataba ya udhamini wa ligi
kuu ya soka ya Zanzibar (ikiliwa ni mkataba wa miaka mitatu) kupitia
kinywaji cha Grand Malt wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kisiwani
Zanzibar.Katikati ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mh. Abdallah Hassan
Jihad.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar,Mh. Ally Mbarouk (wa tatu kushoto) akikadhi Mkataba huo kwa
Kaimu Rais wa ZFA,Ally Mohamed (wa pili kulia) ukiwa ni mkataba wa miaka
mitatu ya udhamini kutoka kwa TBL kupitia Kinywaji chake cha Grand
Malt wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kisiwani Zanzibar.Wengine
pichani toka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,Kushilla
Thomas,Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mh. Abdallah Hassan Jihad na kulia ni
Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam.
Kinywaji
maarufu cha Grand Malt leo kimethibitisha rasmi kudhamini ligi kuu ya
soka visiwani Zanzibar kwa msimu utakaonza mwezi Agosti mwaka 2012.
Akizungumza
katika makabidhiano ya mkataba wa udhamini huo yaliyofanyika katika
hoteli ya Bwawani, Zanzibar; Meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi
Consolata Adam alisema; Grand Malt ni kinywaji kisicho na kilevi,
ambacho kimetokea kupendwa sana na watumiaji kote Tanzania Bara na hapa
Zanzibar.
Leo
tunayo furaha kubwa sana kutangaza kuwa kinywaji hiki mkipendacho cha
Grand Malt kimekubali kwa heshima na taadhima kuchukua jukumu la
kuendeleza soka la Zanzibar kwa kudhamini Ligi kuu ijulikanayo kama
“Zanzibar Premier League”.
Kwetu
sisi, hii ni mojawapo ya njia tutakazozitumia kurejesha fadhila zetu
kwa wazanzibari kwani mmekipokea kinywaji hiki na kinaendelea kukua kwa
kasi, nasi hatuna budi kusema Ahsanteni sana kupitia ushirikiano huu
tunaouanza katika kuhakikisha tunaendeleza soka la Zanzibar kupitia
udhamini huu.
Akielezea
udhamini huo, meneja masoko wa Grand Malt Bw. Fimbo Butallah alisema;
Tumesaini mkataba wa miaka mitatu kuidhamini ligi kuu ya Zanzibar
kupitia kinywaji cha Grand Malt. Mkataba huu unaanza mwaka huu 2012 kwa
msimu wa ligi utakaoanza mwezi Agosti hadi mwaka 2014.
Kwa
mwaka huu wa kwanza Grand Malt itatoa shilingi 140,000,000/- ambapo
fedha hizi zitatumika kwa mahitaji mbali mbali ya ligi kama vile
mahitaji ya Timu shiriki kwa usafiri, chakula na malazi, vifaa vya
michezo na zawadi kwa washindi.
Kufuatia
udhamini huu ambao ni zaidi ya asilimia 70 ya mahitaji ya kuendesha
ligi, sasa Grand Malt inawaasa wadau wote wa soka hapa Zanzibar
kushirikiana kwa pamoja ili tuhakikishe kuwa tunaleta mabadiliko makubwa
katika tasnia hii.
Nae
Makamu wa Raisi wa Chama cha Mpira Zanzibar (ZFA); Bw. Ally Mohamed
alisema; Tukio hili la leo ni matunda ya mchakato mzima ulioongozwa na
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo ya Zanzibar na uongozi wa
Chama cha mpira Zanzibar (ZFA).
Ambao
walitoa fursa hii kwa Grand Malt, kuweza kudhamini ligi yetu ya
Zanzibar. Fursa hii inatokana na ukweli kwamba hawa wenzetu wana uzoefu
mkubwa katika kuendeleza soka na michezo mbalimbali. Kwa Udhamini huu
Grand Malt sasa inapewa heshima ya kubeba jina la ligi hii na hivyo
itajulikana kama “Grand Malt Premier League”.
Tuna
imani kubwa kuwa ushirikiano huu tunaouanza sasa na Grand Malt utaleta
ufanisi mkubwa katika ligi yetu. Kwa niaba ya ZFA tunaahidi kuzingatia
masharti na matakwa ya mkataba, na kutoa ushirikiano thabiti katika
kuendeleza michezo hapa Zanzibar.
Pia
tunatoa fursa kwa wadau wengine kujitokeza ili wachukue nafasi ya
wadhamini wenza ili kuongeza nguvu zaidi katika hiki tulichopata toka
Grand Malt.
No comments:
Post a Comment