Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, April 27, 2012

FRANCIS CHEKA NA MADA MAUGO WAPIMA UZITO TAYARI KWA MPAMBANO WAO



WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wamewapima uzito   na bondia  Mada Maugo  na  Na Francis Cheka wote wamekutwa na kilogramu 76.5 ambapo mpambano wao utafanyika Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.
 
“Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D.

No comments:

Post a Comment