(NA
VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO)
DAR
ES SALAAM
Haraiki ya wanafunzi wapatao 1,727 kutoka shule za msingi mbalimbali Tanzania bara na visiwani wameipamba vizuri sherehe ya maadhimisho ya
miaka 48 ya Muungano wa Tanzania
yaliyofanyika leo katika viwanja vya Uhuru
jijini Dar es Salaam.
Kati ya wanafunzi hao, ni
wanafunzi 727 ambapo 500 wanatoka Tanzania bara, 200 Tanzania visiwani na 27 ni
mahodari wa kucheza sarakasi ambao waliingia uwanjani na kutengeneza maumbo
mbalimbali pamoja na kuimba wimbo maalumu uitwao Uamuzi wa Busara.
Maumbo yaliyotengenezwa na
haraiki hiyo ni pomoja na bendera ya taifa, herufi zenye umbo la miaka 48 ya Muungano, na maumbo
ambayo ndani yake walicheza salakasi na ngoma za asili za ndalandala kutoka Tanzania bara na chaso kutoka Zanzibar.
Maumbo mengine ni pamoja na
madini ya Tanzanaiti ambayo hayapatikani sehemu yoyote duniani zaidi ya Tanzania na maumbo ya mazao ya uchumi ya katani
na pamba yanayolimwa Tanzania
bara na karafuu Tanzania
visiwani.
Haraiki hiyo imeandaliwa na
ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na
wakufunzi wake ni Kilema Athuman Kambangwa akisaidiwa na Mwalimu Grace Ernest
Kabohora kutoka shule ya msingi Wailesi katika manispaa ya Temeke.
Katika maadhimisho hayo Mgeni
rasmi alikuwa ni Rasi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
na kauli mbiu ni “Shiriki kikamilifu katika Sensa na mchakato wa Mabadiriko ya
Katiba”.
No comments:
Post a Comment