Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemuondoa
mwamuzi Rashid Msangi wa Dodoma kwenye orodha ya waamuzi kwa kuvuruga
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyochezwa
Aprili 23 mwaka huu.
Pia
waliokuwa waamuzi wasaidizi wa mechi hiyo; Samuel Mpenzu na Abdallah
Uhako wote kutoka Arusha nao wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa
Ligi Kuu ya Vodacom.
Vilevile
Kamati imeipa Azam ushindi wa mabao 3-0 kwa mujibu wa Ibara ya 31 ya
Kanuni za Nidhamu za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Kwa mujibu wa kanuni hiyo, timu itakayohesabika kupoteza mechi (Mtibwa
Sugar) itakuwa imefungwa mabao 3-0.
Kwa
mujibu wa Kanuni ya Ligi Kuu ya Vodacom kifungu cha 22(3-6) Mtibwa
Sugar imepigwa faini ya sh. 500,000, imepoteza mapato yote ya mchezo huo
na inatakiwa kulipa faini hiyo kabla ya mechi inayofuata.
Nao
makamishna watatu; Abdallah Mitole wa Dar es Salaam, William Chibura
(Musoma) na Omari Mawela (Mwanza) wameondolewa kwenye orodha ya Ligi Kuu
ya Vodacom kwa kushindwa kufika kwenye mechi walizopangiwa kusimamia
bila taarifa.
Makamishna
hao wametakiwa kutoa maelezo ya maandishi wakieleza sababu za kutofika
kwenye mechi. Mechi walizokuwa wamepangia ni Coastal Union vs Ruvu
Shooting (Mitole), Kagera Sugar vs Yanga (Chibura) na Kagera Sugar vs
African Lyon (Mawela).
Nayo
Moro United imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya wachezaji wake
kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadirishia (dressing rooms) wakati wa
mechi namba 171 kati yao na Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 8(16).
Pingamizi
la Villa Squad dhidi ya African Lyon kuwa wakati wa mechi yao ilitumia
wachezaji wawili (Mohamed Samata na Benedict Jacob) ambao mikataba yao
imemalizika limetupwa kwa vile wana leseni halali za kucheza ligi.
Pia
mwamuzi wa mechi namba 160 kati ya Moro United na Oljoro JKT, Nathaniel
Lazaro wa Kilimanjaro amefungiwa miezi sita na kuondolewa kwenye orodha
ya waamuzi kwa kutozingatia kutunza muda kwa mujibu wa kanuni ya
26(1)(f).
Vilevile
Kamishna wa mechi ya Moro United na Oljoro JKT, Ali Mkomwa wa Pwani na
Said Mnonga wa Mtwara aliyekuwa mwamuzi msaidizi mechi kati ya Villa
Squad na Coastal Union wameandikiwa barua za onyo wakitakiwa kuwa makini
kwenye michezo wanayosimamia.
No comments:
Post a Comment