skip to main |
skip to sidebar
KAMATI KUU YA CCM YABARIKI RAIS JAKAYA KIKWETE KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya
wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya
kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.
Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu
na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya
jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na
watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika
na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa
hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.
Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge
kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali
kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za
serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.
2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki
uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine
zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo
ufanywe mapema iwezekanavyo.
Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule
ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika
sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.
Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza
la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu
inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na
kuanza kuifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment