Mashindano
ya kumtafuta Miss Ukonga 2012 kitongoji cha jijini Dar es Salaam,
yanendelea kwa kasi katika Ukumbi maarufu Hiltec uliopo Ukonga, Banana,
jijini Dar es Salaam ambapo warembo hao wanadai kila moja atakuwa
mshindi katika shindano hilo.
Mazoezi
hayo yalishuhudiwa na Miss Tanzania wa sasa, Salha Israel, na
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga. ambao walitoa
ushauri kadhaa kwa warembo hao.
Fainali ya mazoezi hayo itafanyika Mei 5 mwaka huu katika Ukumbi wa Wenge Guarden ulipo Ukonga FFU.
PICHA NA GPL
No comments:
Post a Comment