Awali,
wabunge hao walilazwa katika Hospitali ya Rafaa Bugando lakini baadaye
walisafirishwa kwa ndege kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), Dar es Salaam. Kwa upande wake, Waziri amelazwa
Bugando.Kamanda Barlow alisema katika vurugu hizo magari matatu likiwemo
la Kiwia yaliharibiwa.
Majeraha aliyopata kichwani mh.Highness Kiwia
Majeraha mgongoni mwa mh. Highness.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mabina amekana wafuasi wake kuhusika na uvamizi huo dhidi ya wabunge hao, akidai kwamba pengine wabunge hao walikutana na wahuni au majangili wakawavamia na kuwashambulia kwani mazingira ya usiku namna hiyo huwezi kuamini kwamba CCM wamefanya shambulio hilo nakuwataka wabunge hao wahojiwe zaidi walikwenda kufanya nini maeneo hayo nyakati hizo.

Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow alisema juzi kwamba mbali
na wabunge hao, Samson Highness Kiwia wa Ilemela (kushoto) na Salvatory
Machemuli wa Ukerewe (kulia) PICHANI, wengine walioshambuliwa ni
pamoja na Ahmed Waziri ambaye inasemekana kuwa ni kada wa UVCCM
aliyekatwa kiganja chake cha mkono wa kulia.
Wengine ni Haji Mkweda (21), ambaye alijeruhiwa mguu wa kulia, Judhith Madaraka (26), aliyechomwa kisu kwenye titi lake la kushoto na mkono wa kushoto, Ivory Mchimba (26), aliyejeruhiwa kichwani na mdomoni. Majeruhi wote ukiondoa wabunge hao na Waziri, wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.
Picha na Habari na Mdau Albert G.Sengo

No comments:
Post a Comment