watu wenye ulemavu wa ngozi wakiingia katika viwanja vya Mnazi Mmoja
kumalizia maandamano yao yaliyoanzia katika viwanja vya Leaders jana,
maandamano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Badef kwa lengo la kuchangisha
fedha za kusaidia albino nchini
Mbunge wa viti maalum
Viti Maalum Mh.Shaimaar Kwegyr akisalimiana na washiriki wa maandamano
hayo mara baada ya kufika katika viwanja vya Mnazi mmoja leo.
Shilingi milioni mbili zimekusanywa
katika Harambee ya kusaidia kampeni ya kufanikisha maendeleo ya watu
wenye ulemavu wa ngozi nchini iliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi
Mmoja.
Waliochangia fedha hizo ni Waziri wa
Afya na Usatwi wa Jamii Mh.Dkt. Hadji Mponda aliyetoa milioni moja,Meya
wa Manispaa Kinondoni Ndg.Yusuph Mwenda alitoa laki tano huku Mbunge wa
Viti Maalum Mh.Shaimaar Kwegyr akitoa laki tano.
Akizungumza
na watu waliojitokeza katika matembezi hayo Mwenyekiti wa Taasisi
inajishughulisha na maendeleo ya watu wenye ulemavu iitwayo Badef,
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mh.Salum Barwany ambae Mbunge wa Lindi Mjini alisema kuwa shilingi milioni 500 zinahitajika.
Mh.Barwany
alisema kuwa walemavu wa ngozi wanakabiliwa na tatizo la kansa ya ngozi
ambayo inawashika kiurahisi zaidi kutokana na ngozi yao hivyo fedha
hizo zitasaidia kuwanunulia mahitaji muhimu watu hao.
Alisema kuwa pia
wanakabiliwa na tatizo la elimu kwa kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi
wana tatizo la kuona mbali hali inayowafanya kushindwa kuona vema
darasani hivyo wanahitaji msaada maalum.
Alisema kuwa hizo ni moja kati ya
changamoto ambazo jamii inatakiwa kuwasaidia walemavu hao kukabiliana
nazo ambapo ili kufanikisha hilo kuna haja ya kufanya utafiti.
Alisema kuwa fedha hizo zitasaidia
kufanya utafiti wa kubaini namna ya kuwasaidia watu wenye ulemavu wa
ngozi katika nyanja za elimu, kijamii na hata uchumi.
Pia Mh.Barwany alisema
kuwa fedha hizo zitasaidia kuwasafirisha kiurahisi albino ambao
watakuwa na dalili za kansa ya ngozi ili kuwahi katika hospitali za
rufaa kwa ajili ya matibabu.
“ Kwa sasa sisi walemavu wa ngozi
tunahitaji milioni 500 ili angalu tuweze kusimamia na kujipatia mahitaji
yetu muhimu ya kiafya hapa nchini, hivyo wanajamii tunaomba tusaidiane
katika hilo tafadhali” alisema Barwany.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alitakiwa
kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh.Dkt.Hadji Mponda ambae
hakuwepo na hivyo aliwakilishwa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph
Mwenda.
Maandamano yalianzia Viwanja vya Leaders na kumalizikia viwanja vya Mnazi Mmoja.
Vilevile
unaweza kuchangia kupitia: Mpesa Namba; 0769696999, Airtel Money Namba;
0688858535, TigoPesaNamba; 0655029595 au kwenye akaunti ya BADEF (CRDB
Bank, Lumumba Branch Akaunti Na. 0150278228900).
No comments:
Post a Comment