Mstahiki
Meya wa jiji la Mbeya Athaanas Kapunga leo amewakimbia waandishi wa
habari waliotaaka kumhoji juu ya mgomo wa wafanyabiashara katika soko la
Soweto jijini hapa
Baada
ya meya huyo kukamilisha shughuli ya kuzungumza na wafanyabiashara na
kutembelea miundombinu ya soko hilo wanahabari walimfuata wakitaka
kuzungumza naye lakioni mmoja wa maafisa aliokuwa ameambatana nao Odas
Aron akawaambia amesema atazungumza nao katika ofisi za jiji anakoelekea
muda huo.Wanahabari hao chapchap walitafuta usafiri binafsi na kuanza kufukuzia msafara wa meya lakini kutokana na foleni hawakujua kama walipigiwa chenga wapi na maskini wakaendelea na safari hadi ofisi za jiji na kuambulia patupu.
Baada ya kuuliza waliambiwa msafara huo haujafika ofisini hapo na ndipo ikawalazimu wanahabari kusubiri mpaka waluipokata tamaa,na hata walipojaribu kupiga namba za simu za Meya hazikupatikana huku ofisa aliyewapa maelezo kuwa Meya angezungumza nao ofisini kwake akiwa hapokei
simu.
source chimbuko letu
No comments:
Post a Comment