Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, May 6, 2012

SIMBA YAWACHAPA WATANI WAO WA JADI YANGA MAGOLI MATANO KWA BILA LEO PALE UWANJA WA TAIFA







UBAO WA TAIFA UNAONESHA HIVI 

Mchezaji wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi akishangilia goli mara baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza katika mchezo wa kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom inayomalizika leo kwenye uwanja wa Taifa huku ikiwa tayari ni mabingwa wa ligi hiyo, 
Goli la pili la Simba limefungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache zilizopita tayari Emmanuel Okwi ameongeza goli la tatu , Juma Kaseja ameongeza goli moja wa penati wakati pia Patrick Mafisango amefunga goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari 
Mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi akiwania mpira mbele ya Shadrack Nsajigwa wa Yanga katika mchezao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania inayomalizika leo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiangalia kitu jukwaani haikufahamika lilikuwa ni tukio gani.
Wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Kikosi cha timu ya Simba ambao ndiyo mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2011-2012 kikiwa katika picha ya pamoja na Kocha wao Milovan.
Manahodha wa Simba na Yanga Juma Kaseja kushoto na Shadrack Nsajigwa wakisalimiana mbele ya waamuzi kabla ya kuanza kwa mpambano huo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamefurika uwanjani hapo.

Picha kwa hisani ya FULL SHANGWE



 Wachezaji wa Simba wakishangilia na Kombe mara baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom iliyomalizika jana Uwanja wa Taifa dhidi ya watani wao wa jadi Yanga.Simba ilishinda 5-0.


 Wachezaji wa Simba wakishangilia na Kombe


 Mashabiki wa Simba wakishangilia kwa namna yake


 Wachezaji wa Simba wakitembea mithili ya Simba mara baada ya kuwafunga watani wao wa jadi Yanga wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa  kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana.Simba ilishinda 5-0.Mbele ni Mchezaji wa timu hiyo, Uhuru Selemani na motto wake


 Wachezaji wa Simba wakishangilia


 Waziri wa Habari akimkabidhi Kombe nahodha wa Simba Juma Kaseja mara baada ya kutwaa Ubingwa  timu ya Simba


Mashabiki wakishangilia kwa mbwembwe
Picha zote na Kamanda wa matukio Blog

No comments:

Post a Comment