Balozi
wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela, akikabidhi Hati
za utambulisho kwa Mh. Giorgio Napoletano, Rais wa Jamhuri ya Italy,
jana tarehe 19 Juni 2012 saa 11.10 jioni katika kasri ya Rais
ijulikanayo kama ‘Quirinale’.
Mh. Giorgio Napoletano, Rais wa
Jamhuri ya Italy, akimkaribisha Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng.
Dr. James Alex Msekela, katika kasri yake iliyopo kati kati ya mji wa
Rome. Kasri hiyo inajulikana kama ‘Quirinale’. Pamoja na Mh. Napoletano,
walikuwepo pia; Mkuu wa Itifaki katika kasri hiyo, na washauri wengine
wa Rais wa Italy.
Rais wa Jamhuri ya Italy, Mh. Giorgio
Napoletano, akipitia Hati za utambulisho wa Balozi wa Tanzania nchini
Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela. Baadaye Mh. Rais alimkaribisha
Balozi ofisini kwake kwa mazungumzo mafupi.
Balozi wa Tanzania nchini Italy pia ndiye mwakilishi wetu katika nchi za Ugiriki, Uturuki, Slovenia, Croatia, Serbia, Malta, Bosnia na Herzegovina, na Albania. Katika uwanda wa mashirikiano mapana ya kimataifa, Balozi huyu pia anaiwakilisha Tanzania katika FAO, WFP na IFAD, ambayo yote ni mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) yenye makao yake makuu mjini Rome.
JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA INAUNGANA NA SERIKALI YA ITALIA KWENYE KUMKARIBISHA NA KUMPONGEZA ENG. DR. JAMES MSEKELA NCHINI ITALIA. JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA PIA INAAIDI KUSHIRIKIANA NA MH. BALOZI KWENYE MASWALA MBALI MBALI YA KUJENGA TAIFA LETU LA TANZANIA.

No comments:
Post a Comment