Mwanamuziki na producer anayemiliki studio ya Sharobaro Records, Bob
Junior aka Mr. Chocolate Flava, ameamua kufungua ndoa kwa style ya aina
yake.
Amesema harusi yake itakayofanyika jumapili ya tarehe moja mwezi July
mwaka huu, pamoja na kufanyika nyumbani itatinga ndani ya club ya
Billicanas ambapo kila mtu anaruhusiwa kuhudhuria.
Rais huyo wa masharobaro amesema wiki hii atapanda boti hadi Zanzibar
kwenda kumfuata ‘mwali’ ili aisaliti rasmi kambi maarufu ya makapela.
Bob Junior anayesifika kwa kukata ‘mauno’ kwenye video zake, amesema
amechoka kuishi maisha ya ujana na sasa anahitaji kuwa na familia.
“Tunapiga show kila siku na kupata hela nyingi kwanini nisioe,” aliiambia 255 ya Clouds Fm jana.
Aliongeza kuwa dhumuni la kuamua kuoa ni kuepukana na vishawishi na
maradhi kwakuwa watu maarufu kama yeye hujikuta wakitafutwa sana na
wasichana.
.
No comments:
Post a Comment