Aliyekuwa mwimbaji wa bendi ya Machozi inayomilikiwa na mwanadada Lady
Jaydee amesema sababu za kujiondoa kwenye bendi hiyo ni kutokana na
ubabaishaji mkubwa unaoendelea.
Akiongea na Clouds Fm jana, Mwinyi amesema hakufukuzwa kwenye bendi hiyo
bali aliamua kuondoka mwenyewe baada ya kuchoshwa na ahadi za uongo
kutoka kwa uongozi wa bendi hiyo.
Amesema kuwa kwa muda mrefu ameuvumilia ule aliouita ‘mkataba wa
kijinga’ aliokuwa anautumikia kwa malipo ya kila mwisho wa wiki ambayo
hata hivyo yalikuwa kiduchu na wakati mwingine alikuwa hakuti bahasha
yake.
Mwinyi ambaye pia ni model, alieleza kuwa pamoja na bendi nyingi
kutangaza nia ya kumchukua kwa ahadi za mkwanja mrefu, aliendelelea
kuuvumilia ‘uswahili’ wa Machozi bendi na heshima yake kwa Lady Jaydee
huku akiimba ‘for fun tu’.
Amesema Lady Jaydee alikuwa akimwonesha dharau kubwa na kujiona yuko juu
wakati bendi yakeisingefika hapo ilipo bila ya mchango wake.
Mwimbaji huyo aliongeza kwa kusema kuwa sifa za nje za bendi hiyo ni
kubwa lakini ukweli wa ndani ni kuwa haina lolote zaidi ya uswahili na
ubabaishaji mwingi.
Mwinyi si msanii pekee aliyejitoa hivi karibuni kwenye bendi hiyo ya Machozi.
Mwimbaji mwingine aitwaye Sam ameamua kwenda kutafuta riziki kwenye
bendi ya Skylight inayomilikiwa na mshiriki wa zamani wa Tusker Project
Fame,Aneth Kushaba kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi
milioni sita.
Clouds Fm walipojaribu kumpigia simu Gadner Habash kuelezea masuala hayo aliwapa jibu la ‘NO COMMENT’.
No comments:
Post a Comment