Rapper mdogo kutoka A town Dogo
Janja aliekua akisoma na kuishi Dar es salaam amerudishwa kwa wazazi
wake Arusha jana kutokana na kufanya mambo mbalimbali ambayo uongozi wa
Tiptop Connection haujapendezwa nayo.
Tip Top ambao walikua
wanasimamia kazi za muziki za Janja wamempandisha basi na kumrudisha
kwao juzi baada ya kuona msanii huyo hazingatii shule kama inavyotakiwa,
amekua mtoro wa mara kwa mara katika shule aliyokua akisoma ya Makongo
na hasikii anaporekebishwa, hiyo ndio sababu kubwa ya kumrudisha ili
kukwepa lawama za baadae ambazo zingetokana na Dogo Janja kutosimamiwa
vizuri kwenye swala la Elimu kwa sababu Tiptop ndio waliokabidhiwa
kumsimamia.
SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA UWEKEZAJI NA UKUAJI WA UCHUMI
-
*Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati
akifungua Mkutano wa Majadiliano ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na
Washirik...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment