Gari la wangonjwa la AAR ambalo lilimbeba Dk. Ulimboka likiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Baadhi
ya wanaharakati na wauguzi wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa
kulaani kitendo cha kikatili alichofanyiwa daktari huyo.
Mwenyekiti
wa Jumuia ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka leo mchana
alifikishwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya
kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya madaktari
kubaini kuwa ana mtatizo ya kitabibu yanayomkabili likiwemo la mtikisiko
wa ubongo.
Mwenyekiti
huyo alifikishwa uwanjani hapo majira ya saa 8.30 na ndege aliyosafiri
nayo iliondoka saa 10.15. Uwanjani hapo kulikuwa na wanaharakati ambao
walikuwa na mabango, kinyume cha matarajio ya wengi walizani kuwa
angeteremshwa na kuingizwa na machela Uwanjani hapo lakini gari
lililombeba lilipita moja kwa moja hadi ndani ya uwanja huo.
No comments:
Post a Comment